DAR ES SALAAM :MEYA wa Manispaa ya Temeke Dar es salaam Abdallah Mtinika amekabidhi madawati 6,000 kati ya madawati 3,000 kwa Afisa Elimu awali na msingi wa Wilaya hiyo amabapo yanatengenezwa na fedha zilizotokana na mapato ya ndani lengo likiwa ni wanafunzi wapate elimu bora kwa maendeleo ya Taifa.
Madawati yatatumika kwenye shule zote 89 za msingi zilizopo katika wiliya hiyo hayo ameyasema leo Meya huyo wakati wa uzinduzi wa madawati hayo kwenye shule ya msingi Wailes iliyopo Manispaa ya Temeke hivyo madawati hayo yatatatua kero ya wengi wa wanafunzi wengi kwenye changamito hiyo ya madawati.
Abdalla amesema madawati yote yakitengenezwa yapelekwe sehemu zilizokusudiwa lengo kama halmashauri ni kupunguza hilo tatizo la la upungufu wa madawati lililopo kwenye shule hizo.
“Madawati haya 6,000 yaanze kusambazwa alafu tutaendelea kuona bado upungufu upo wapi ili tuzidi kuyaongeza kwa hiyo tulizindua kwa shule za sekondari na leo ninazindua mpango wa madawati 6,000 kwenda kwa shule za msingi za wilaya Temeke.
“Niwaombe katika ugawaji huu watumishi wetu mpeleke madawati haya katika maeneo yenye uhitaji lengo letu hatutaki watoto wakae chini wanachafuka lakini hawapati eliku sahihi kwa hiyo naamini mpango wa kugawa upo shule hizi kabla ya kuzitengeneza madawati uhitaji mmeshautambua malengo yetu kama halmashauri tatizo likapungue au kumalizika kabisa ” amesema Abdallah.
Kwa upande wake Mshana Samwel Kawia Afisa elimu awali na Msingi Wilaya ya Temeke amesema madawati hayo yatakwenda kupunguza tatizo walilonalo katika Manispaa yao ya Temeke kwa sababu ina wanafunzi 139,434 huku baadhi ya wanafunzi wakiwa wanakaa chini na vyumba vya madarasa ni vichache.
“Chumba kimoja kinatakiwa kiwe na madawati 15 tuu lakini darasa hilo linalazimika kuwa na wanafunzi mpaka 70/80 kwa hiyo utengenezaji wa madawati unaendana sambamba na ujenzi wa vyumba vya madarasa ambayo halmashauri ya temeke inafanya kwa kasi kubwa kwa mapato ya ndani .
” Utengenezaji wa madawati huu utaongeza ufaulu kama tunavoona darasa la nne tulikuwa na asilimia 96 darasa la saba 94 naamini mtoto anapokaa kwenye dawati anafanya vizuri zaidi” amesema Mshana.
Kwa upande wake Evetha Karani Mkuu wa Shule ya msingi Wailes ameshukuru kwa msaada huo wa madawati na kusema kuwa utaenda kutatua kwa kiasi kikubwa changamoto ya madawati shuleni hapo
Naye Marium Mtemvu Diwani viti maalum mwenyekiti huduma za jamii manispaa ya temeke amesema kwenye halmashauri hiyo walikuwa na changamoto juu ya madawati hivyo itasaidia wanafunzi kupata elimu bila changamoto.