TET yatoa elimu matumizi ya vitabu vya nukta nundu

TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) imeendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi ya nukta nundu (BRAILLE) kwa masomo ya wanafunzi wasioona.
TEA inatoa elimu hiyo katika maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Saba Saba) lengo ni kuongeza uelewa kwa jamii.
Mhakiki wa maandishi ya nukta nundu wa TET, Hadija Salum amesema jamii inahitaji kuelewa vitabu hivyo na vifaa mbali mbali wanavyotumia wasioona na wale wenye uoni hafifu.
“Tunaonesha vitabu vya maandishi ya wasioona ambayo wanatumia wanafunzi na walimu wasioona pia hii ni katika elimu ya awali, shule za msingi, sekondari na na vyuo vya ualimu,” amesema Salum.
Amebainisha kuwa mahitaji mengine ya wasioona ni matumizi ya fimbo, ubao wa kujifunza alfabeti na ubao wa namba.
“Mbali na braille TET tunaandaa vitabu vya maandishi yaliyokuzwa (large print) kwa ajili ya wanafunzi wenye uoni hafifu hivyo vifaa vyote vipo hapa na tunatoa elimu kwa watu wote,” ameeleza.
Kadhalika, TET ina vifaa vingine ikiwemo karatasi za michoro mguso kitaalamu ‘brelon’ kwa wasioona na kalamu ya kuandikia watu wasioona inayojulikana kama Stylus.
Salum ameishukuru serikali kwa kufanikisha vitabu vya kutosha kwa hatua hiyo kwamba walengwa watapata mahitaji ya kutosheleza kwa shule zote.
TET imechapisha vifaa na vitabu vya Kidato cha kwanza hadi sita vya Braille na Maandishi kwa ajili ya mwanafunzi wenye mahitaji maalumu ya kutokuona na uoni hafifu vikichapwa katika uwiano wa vitabu vitatu kwa mwanafunzi mmoja (3:1).
Vitabu, hivyo ni vya masomo ya Jiografia, Kiswahili, Uraia, Kilimo, Kiingereza, Histori, Biolojia, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Hisabati.
Vitabu hivyo vinawawezesha wanafunzi wenye mahitaji maalumu ya uoni kujifunza kama ilivyo kwa wanafunzi wengine na kupata stadi na umahiri utakaowasaidia kumudu changamoto mbalimbali wakati wa kujifunza.
Mpaka sasa vitabu hivyo vimesambazwa katika shule 764 za wanafunzi wasioona na wenye uoni hafifu Tanzania Bara na Zanzibar.




I’m not sure where you are getting your info, but good topic.
I needs to spend some time learning more or understanding more.
Thanks for great information I was looking for this info for my mission.
When I originally commented I appear to have clicked on the -Notify me when new comments are added- checkbox and now every time a comment is added I receive 4
emails with the same comment. Is there an easy method you are able
to remove me from that service? Cheers!