TFS yatatua migogoro ya mipaka na vijiji kwa 96%

MOROGORO: WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umefanikiwa kutatua migogoro ya mipaka 423 kati ya 438 iliyokuwa inahusiana na vijiji na wadau wengine iliyoanishwa kupitia kamati ya mawaziri wanane iliyoundwa na hivyo kusalia migogoro 15.

Kamishna wa Uhifadhi wa TFS, Profesa Dos Santos Silayo amesema hayo kwenye taarifa yake mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamad Hassan Chande kabla ya kufungua mkutano wa nne wa Makamanda, maofisa na askari uliofanyika mjini Morogoro.

Profesa Silayo amesema chini ya maelekezo ya Rais kupitia Kamati ya Mawaziri nane katika kipindi cha hivi karibuni imeweza kutatua migogoro mingi Kwa kiwango Cha asilimia 96 iliyokuwa inaikabili misitu yetu.

Kamishna wa Uhifadhi wa TFS alisema katika kutekeleza maelekezo hayo na yale yaliyotiolewa wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Ushauri Wakala ulihakikisha maeneo ambayo migogoro imetatuliwa, uvamizi wa misitu au migogoro mipya haijitokezi tena.

“Tutahakikisha kwa kushirikiana na Mamlaka nyingine tunamaliza kabisa utatuzi wa migogoro 15 iliyobakia na juhudi zinaendelea kuimaliza,” amesema Profesa Silayo.

Akifungua mkutano huo ,Naibu Wizara ya Maliasili na Utalii ,Chande ameutaka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kuongeza kiwango cha uzalishaji wa asali kutoka tani 9.5 inayouzwa nje ya nchi kwa mwaka na kufikish tani 50,000 Kwa mwaka.

” Kiwango hiki kinaweza kuongezeka endapo Wakala kupitia Wataalamu waliopo watatumia rasilimali za misitu kwa kuwa Kuna makundi ya nyuki Zaidi ya milioni tisa”amesema Chande.

Chande amesema asali ya Tanzania imepata soko kubwa nchi za nje kutokana na ubora wake ,hivyo Wakala unapaswa kuongeza juhudi katika kuongeza uzalishaji ili kuongeza kiwango cha mauzo ya nje na kuingiza fedha za kutoka kwa wakala na Serikali.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TFS, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa amesema Bodi itaendela kusimamia utekelezaji wa maamuI na kutoa ushauri wa kitaalam Ili kuimarisha mifumo ya utatuzi wa migogoro kwa la Kuzuia changamoto hizo kutojitomeza siku zijazo.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site

  2. I get paid over (90$ to 200$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $18000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ https://Www.Cash54.Com

  3. I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button