THRDC yaomba msaada kumpata Twaha Mwaipaya

DAR ES SALAAM: MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umeiomba Serikali ya Kenya kushirikiana na Tanzania kufuatilia taarifa za kutoweka kwa mwanaharakati Mtanzania Twaha Mwaipaya, ambaye hadi sasa hajulikani alipo.

Katika taarifa iliyotolewa na Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa, mtandao huo umesema umesikitishwa na taarifa za kutoweka kwa Mwaipaya, anayedaiwa kuonekana mara ya mwisho Jumapili, Oktoba 25, 2026, akiwa katika maeneo ya nje ya jiji la Nairobi.

Mamlaka nchini Kenya zimetupilia mbali madai kuwa Mwaipaya amepotea nchini humo katika mazingira ya kutatanisha. Wakati huo huo Jeshi la Polisi nchini Tanzania (bado halijatoa taarifa yoyote kuhusiana na madai hayo.)

THRDC imeziomba mamlaka husika kufanya uchunguzi ili kubaini alipo Mwaipaya na kuthibitisha mazingira ya kutoweka kwake.

Mtandao huo umesema Katiba ya Kenya ya mwaka 2010, ikiwemo Ibara za 21(1), 26 na 29, inaweka masharti kuhusu wajibu wa Serikali kulinda haki za msingi, haki ya kuishi na usalama wa watu.

THRDC pia imeiomba Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kupitia ubalozi wa Tanzania nchini Kenya kusaidia upatikanaji wa taarifa sahihi za alipo Mwaipaya.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button