Timu 14 za bodaboda kuwania mil 3/-

TIMU 14 za waendesha bodaboda katika Manispaa ya Kigoma Ujiji na Buhigwe zimeanza mashindano ya ya mpira wa miguu kuwania Sh milioni 3 Ligi ya Bodaboda inayoendeshwa na kituo cha Radio cha Main FM cha mjini Kigoma.

Mkurugenzi wa Kituo cha Radio Main FM, Paschal William amesema kuwa mashindani hayo yanayofanyika uwanja wa Kawawa Ujiji mjini Kigoma. Aidha, pamoja na zawadi hizo pia wachezaji wote na mabenchi yao ya ufundi watafaidika na mafunzo ya ujasiliamali, usalama barabarani, nishati safi na afya.

Steven Ndorobo Msemaji wa mashindano ya Main FM yanayofanyika Kigoma Mjini

William amesema mshindi wa kwanza ataondoka na zawadi ya Sh milioni 1.5, mshindi wa pili Sh milioni 1 na mshindi wa tatu ataondoka na Sh 500,000 na kwamba mashindano hayo yanalenga kutoa ujumbe kwa jamii kwamba bodaboda ni kazi ya maana kama zilivyo kazi nyingine.

Katika mchezo wa ufunguzi timu ya Kombaini ya kijiji cha Mnanila Wilaya ya Buhigwe imeitoa timu ya Kombaini ya Bangwe kwa kuifunga penalti 3-0 baada ya dakika 90 kufungana mabao 1-1.

Timu ya kombaini ya kijiji cha Mnanila Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma iliyocheza mchezo wa ufunguzi

Aidha, msemaji wa mashindano hayo, Steven Ndorobo amesema kuwa pamoja na fursa mbalimbali zilizotolewa kwenye mashindano hayo pia wamewaalika viongozi wa timu mbalimbali kuangaalia vipaji vya wachezaji kuweza kusajili wachezaji watakaoona wanawafaa.

Kikosi cha timu ya Bangwe FC ya mjini Kigoma iliyokuwa ya kwanza kutolewa kwenye mashindano ya Main FM Cup mkoani Kigoma

Ndorobo amesema kuwa mashindano hayo yatakuwa yanaendeshwa kwa mtindo wa mtoano na yatakuwa yanafanyika kila mwishoni wa wiki kwa michezo miwili kupigwa kila wiki na kwamba mashindano hayo yataibua vipaji vingi ambavyo vinaweza kupata nafasi ya kuendelezwa.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Looking for a flexible way to earn extra income? This part-time opportunity allows you to work from home and make $570-$2400 each week. Perfect for anyone wanting to start something new—get your first payment by the end of the week. Tap into Finance, Economy, or Investing to begin!

    Get started here____>> https://Www.earnapp1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button