TIMU ya Bandari Tanga imefanikiwa kupata ushindi wa jumla kwa mchezo wa riadha wanaume kwa kujipatia alama 49 ,wakati wanawake timu ya Bandari Dar es Salaam ikinyakua ushindi wa alama 54.
Msimamizi mkuu wa mchezo wa riadha katika mashindano ya bandari nchini mwaka huu, Leswe Omary alisema Oktoba 29, 2023 wakati ulipofanyika mchezo wa ridhaa na mingine ya jadi ikiwemo ya kurusha mkuki, tufe na bao kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Omary alitaja matokeo ya ujumla ya riadha kwa wanaume , mshindi wa kwanza Bandari Tanga kwa kujipatia alama 49 ( Pointi) akifuatiwa na Bandari Dar es Salaam (DAR PORT) kwa kunyakua alama 42 ikifuatiwa na MSCL kwa kupata alama 27 ambapo jumla ya vituo saba vilishirikisha wachezaji wa mchezo huo.
Kwa wanawake kati ya vituo sita vilivyotoa wachezaji , timu ya Bandari Dar es Salaam (Dar Port) imenyakua ushindi wa kwanza kwa alama 54 ikifuatiwa na Zanzibar alama 34 na watatu ni Kampuni ya Huduma za Meli ( MSCL) ikipata alama 19.
Katika mbio za mita 100 wanaume , Eliasi Mtiri kutoka Bandari Tanga alinyakua nafasi ya kwanza kwa kutumia sekunde 11.01 , akifuatiwa na Shaggy Lugua kutioka Tanga aliyetumia sekunde 11.28 ambapo Ramadhan Masoud kutoka Dar Port akitumia sekunde 11.63 ambapo washiriki walikuwa sita.
Mbio za mita 100 wanawake , Sabahi Zahor kutoka Zanzibar alitumia sekunde 14.80 , Anna Chale kutoka Dar Port alitumia sekunde 15.46 wakati Shani Chogero kutoka Kampuni ya Huduma za Meli ( MSCL) alitumia sekunde 17.30 ambapo washiriki walikuwa watano.
Katika mbio za mita 200 wanaume, Shaggy Lugua kutoka Tanga alishika nafasi ya kwanza alitumia sekunde 23.40 , akifuatiwa na Elias Mtiri kutoka Tanga alitumia sekunde 24.51 na watatu ni Ramadhani Masoud kutoka Dar Port alitumia sekunde 25.03 na washiriki walikuwa sita.
Kwa mita 200 wanawake mshindi wa kwanza alikuwa ni Anna Chale kutoka Dar Port alitumia sekunde 31 , akifuatiwa na Lita Musa kutoka Dar Port alitumia sekunde 34.57 na mshindi wa tatu Mwanakombo Masoud kutoka Zanzibar alitumia sekunde 36.51.
Katika michuano ya mbio za mita 800 wanaume ,Irafay Pius kutoka Dar Port alinyakua nafasi ya kwanza kwa kutumia dakika 2.16 akifuatiwa na Josephat Maundi kutoka Dar Port aliyetumia dakika 2.
18 akifuatiwa na mshindi wa tatu Evarist Christopher kutoka MSCL aliyetumia dakika 2 .19 ambapo washiriki walikuwa sita.
Kwa upande wa wanawake mbio za mita 800 , mshindi wa kwanza alikuwa ni Anna Chale kutoka Dar Port aliyetumia dakika 3.36 akifuatiwa na mshindi wa pili Asha Mgala kutoka Makao Makuu (HQ) aliyetumia dakikaa 3.44 na nafasi ya tatu ikachukuliwa na Fatuma Haji kutoka Zanzibar aliyetumia dakika 5.11 na washiriki walkikuwa ni watatu .