Timu za Taifa zapishana tu angani

DAR ES SALAAM: TIMU za Taifa za Tanzania zinapishana angani, awali mapema asubuhi timu ya Taifa ya wakubwa @taifastars_ imeondoka kuelekea Morocco kwenye mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Niger utakaochezwa kwenye mji wa Marrakech Jumamosi Novemba 18, 2023.
Wakati dada zao timu ya Taifa chini ya umri wa miaka 20 “Tanzanite” imeondoka leo kuelekea nchini Nigeria kwenye mchezo wa marudiano wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Nigeria utakaochezwa Novemba 19, 2023.@tanfootball