TPA yaanza kutekeleza ahadi za Dk Samia Kigoma

KIGOMA: Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) imekabidhi eneo la ujenzi wa soko katika bandari ndogo ya Kibirizi na Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa makandarasi wa mradi huo kampuni ya KGG Investiment Ltd ili kuanza ujenzi wa soko hilo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Samia aliyoitoa mwaka 2022 alipofanya ziara mkoani Kigoma.

Mkurugenzi wa Huduma za Uhandisi TPA, Erick Madinda alisema hayo wakati mamlaka hiyo ikizindua ujenzi wa mradi huo na kumkabidhi mkandarasi wa mradi huo Kampuni ya KGG Investiment Ltd eneo la ujenzi ili mradi huo uanze kutekelezwa.

Mhandisi Madinda alisema kuwa kiasi cha Sh bilioni 6.4 kimetolewa na serikali kwa ajiili ya utekelezaji wa mradi huo ambapo pamoja na soko pia kitajengwa kituo cha polisi huku mradi huo ukitarajia kutumia miezi 12 katika utekelezaji wake.

Mkurugenzi wa Huduma za Uhandisi Mamlaka ya usimamizi wa bandari nchini (TPA), Erick Madinda (kulia) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya Kigoma Rashid Chuacha (wa tatu) Kigoma kuhusu mradi wa ujenzi wa soko na kituo cha polisi katika bandari ndogo ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji mradi wenye thamani ya Sh bilioni 6.4.

Akitoa maelezo wakati wa hafla hiyo Mkuu wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Silvestre Mabula alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo unafuatia ahadi aliyotoa Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara mkoani Kigoma mwaka 2022 ambapo pia alitembelea bandari hiyo na kukuta changamoto ya eneo la awali lililojengwa soko likiwa limezizingirwa na maji kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika wa Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA), Silvestre Mabula akizungumza wakati mamlaka hiyo ikimkabidhi Mkandarasi wa Kampuni ya KGG Investments Ltd eneo la utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa soko na kituo cha polisi katika Bandari Ndogo ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji

Mabula alisema kuwa katika utekelezaji wa mradi huo kutakuwa na maduka na huduma mbalimbali ikiweko vibanda 250 vya maduka, vizimba 250,ofisi, migahawa, maegesho ya magari na maeneo ya vyoo ambavyo vitatumiwa na wafanyabiashara lakini pia kutajengwa kituo cha polisi katika eneo hilo.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Mkuu wa Mkoa Kigoma, Balozi Simon Sirro ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya Kigoma, Rashid Chuachua alisema kuwa ujenzi wa soko hilo katika bandari hiyo ndogo ya Kibirizi utachochea biashara baina ya Mkoa Kigoma na nchi za ukanda wa maziwa makuu, ambazo ni Zambia, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambapo wasafiri wengi wanatumia bandari hiyo kwenda katika nchi hizo.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    .

    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button