TRA Mtwara yawakumbuka watoto yatima

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mtwara imetoa msaada wa vyakula mbalimbali katika vituo viwili vya kulelea watoto yatima na watoto wenye mahitaji maalum katika Manispaa ya Mtwara Mikindani uliyogharimu Sh milioni 12.

Hatua hiyo inakuja ikiwa zimebaki siku mbili kuelekea sikukuu ya Eid El Fitri na Pasaka 2025.

Msaada huo umekabidhiwa leo Machi 28, na Meneja wa TRA mkoani humo, Maimuna Khatibu ambao unaenda kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji zaidi ya 300.

Msaada huo umetolewa katika kituo cha maendeleo ya mtoto na kijana Moravian Mtwara na kituo cha Baraza Kuu la Wanawake wa Kiislam Tanzania tawi la Mtwara vilivyoko kwenye manispaa hiyo.

Kwa upande wake Ofisa Ustawi wa Jamii kwenye manispaa hiyo, Swaum Omary ameipongeza TRA kwa kuwakumbuka watoto hao na wito kwa mamlaka hiyo na wadau kwa ujumla kuendelea kuwakumbuka watoto wenye mahitaji katika jamii.

“Niwaombe wazazi wa manispaa kutowafungia watoto wenye ulemamavu na badala yake wapelekwe katika vituo vya kulelea watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kutimiza ndoto zao”amesema Swaum.

Akitoa shukran kwa TRA Mchungaji Kennedy Kalago kwa niamba ya kanisa la Moravian Usharika wa Mtwara “Tunafuraha kubwa tumeona kama tumetembelewa na malaika,tunashukuru kwa kututhamini”

Katibu wa Baraza la Wanawake wa kiislam Tanzania mkoa wa Mtwara, Aisha Selemani “Wanawake ndio tunaojua changamoto za malezi kwahiyo kwa kuguswa na jambo hilo na kujua matatizo yaliyopo katika malezi hivyo basi tukaamua kuwatafuta  watoto katika kila kata”

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button