TRA yanufaika uhusiano na wafanyabiashara

DAR ES SALAAM: MAKUSANYO ya kodi nchini yamefikia Sh trilioni 24.14 kwa mwaka 2022/23 kutoka Sh trilioni 18.15 mwaka 2020/21 sawa na ongezeko la Sh trilioni 5.99 ikiwa ni mwongozo wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kujenga uhusiano mzuri na wafanyabiashara na kujali changamoto wakati wa kukusanya kodi.

Hii ni kwa mujibu wa tathmini ya mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Samia iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi leo jijini Dar es Salaam.

Katika taarifa yake, Matinyi amesema kwa mwezi Desemba 2023, TRA ilivunja rekodi ya ukusanyaji ya kila mwezi baada ya kufanikiwa kukusanya shilingi trilioni 3.05 licha ya kuwa wastani kwa mwaka huu hadi sasa ni shilingi trilioni 2.13.

Advertisement

“Ni vema kufahamu kwamba hadi kufikia Machi 20, 2024, TRA ilikuwa imeshakusanya kiasi cha Sh trilioni 19.21, ikiwa ni dalili mkwamba itavuka kiasi cha mwaka uliopita,” ameseema Matinyi.

Amesema uwekezaji Katika kipindi mwaka, kuanzia Machi 2021 hadi Machi 2024 Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimefanikiwa kusajili jumla ya miradi 1,188 ambayo ilikadiriwa kuwekeza kiasi cha mtaji wa dola za Marekani milioni 15,041 na kutoa jumla ya ajira 345,464.

“Kati ya miradi hiyo asilimia 35 inamilikiwa na Watanzania, asilimia 41 ni ya Wageni na asilimia 24 ni ya ubia kati ya Watanzania na Wageni,” ameeleza.

Hata hivyo, Kamati ya Kitaifa ya Kusimamia Uwekezaji (National Investment Steering Committee – NISC) ilitoa idhini ya kusainiwa mikataba ya utekelezaji kwa miradi 16.

Miradi hiyo yenye hadhi ya mirahi mahiri ni pamoja na Mradi wa Bagamoyo Sugar Limited; Mradi wa Kagera Sugar Limited; na Mradi wa Mtibwa Sugar Estate Limited;. Vile vile, NISC iliridhia miradi mingine nane ambayo ilisaini mikataba ya utekelezaji na TIC, yaani (perfomance contracts) baada ya kupewa hadhi ya kuwa wawekezaji mahiri maalum.