Transit Camp yaibana Polisi nyumbani

KILIMANJARO: MBIO za kuwania nafasi ya kupanda Ligi Kuu zimeendelea kushika kasi ambapo timu ya Transit Camp imegawana pointi moja katika mchezo wa NBC Championship dhidi ya Polisi Tanzania uliochezwa jana Mjini Moshi.
Mchezo huo umechezwa katika uwanja wa Ushirika Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro ulishuhudiwa ukiwa na upinzani na umakini wa hali ya juu kwa pande zote .
Matokeo hayo yameipandisha Transit Camp hadi nafasi ya nne ya msimamo wa ligi.
Polisi Tanzania waliandika bao dakika 25 lililofungwa na Emannuel Mpuka dakika 25 na wapinzani wao Transit Camp wakisawazisha dakika 45 kupitia kwa Adam Uledi na hadi mpira unamalizika timu hizo zilikuwa zimetoshana nguvu ya goli 1-1.
Matokeo mengine ya Ligi ya NBC Championship yaliishuhudia Mbuni ikishinda goli 1-0 dhidi ya Gunners FC katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Mbeya Kwanza ilishinda 2-1 dhidi ya Kengold, Stand United iliifunga TMA Stars goli 1-0,Bigman ilishinda goli 2-0 dhidi ya Songea United.
Msimamo wa ligi hiyo Geita Gold inaongoza ikiwa imejikusanyia pointi 19, ikifuatiwa na Kagera Sugar pointi 19 kwa tofauti ya magoli, Mbuni Pointi 16 nafasi ya tatu huku Transit Camp FC ikishika nafasi ya nne kwa pointi 12 sawa na Kengold pointi 12 nafasi ya tano huku pia Mbeya kwanza pointi 12 nafasi ya sita zikitofautiana kwa idadi ya magoli.
Ligi hiyo itaendelea tena Novemba 30 kwa michezo mitano kuchezwa katika viwanja vya miji ya mikoa tofauti ambapo Bigman FC dhidi ya Kengold, Mbeya Kwanza dhidi ya Songea United, Stand United itacheza na Mbuni huku Gunners itaivaa TMA na African sport itawakaribisha Transit Camp FC.




I make up to $90 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $40h to $86h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now i am hoping i could help someone else out there by sharing this link…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com