Trump, Netanyahu kukutana White House

WASHINGTON DC : RAIS wa Marekani, Donald Trump, anatarajiwa kuwa mwenyeji wa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, katika mazungumzo yatakayofanyika Jumatatu ijayo kwenye Ikulu ya White House.

Mazungumzo hayo yanajiri wakati Marekani ikiendelea kuishinikiza serikali ya Israel pamoja na kundi la Hamas kufikia makubaliano ya kudumu ya kusitisha mapigano na kukomesha vita vinavyoendelea ukanda wa Gaza.

SOMA: Netanyahu awashutumu viongozi wa Ulaya kuhusu Gaza

Ziara hiyo imethibitishwa na maafisa wa serikali kutoka pande zote mbili, ingawa wamezungumza kwa sharti la kutotajwa majina kwa sababu hawakuruhusiwa kuzungumzia rasmi suala hilo.

Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa Netanyahu kuzuru Washington tangu Trump arudi madarakani Januari mwaka huu, huku ikifanyika katika kipindi nyeti ambacho Marekani imejiingiza moja kwa moja katika mzozo wa Mashariki ya Kati kwa kushambulia maeneo ya nyuklia ya Iran.

Mazungumzo kati ya viongozi hao wawili yanatarajiwa kuangazia hali ya usalama Mashariki ya Kati, kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na kidiplomasia, pamoja na njia za kufanikisha suluhu ya amani ya kudumu kati ya Israel na Palestina.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button