Tshabalala: Haiishi mpaka iishe

DAR ES SALAAM: NAHODHA wa Simba SC, Mohamed Hussein Zimbwe Jr ‘Tshabalala’ amesema kikosi chao bado kina nafasi ya

kufanya vizuri na kufikia malengo ya ķutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).

Kupitia akaunti rasmi ya Instagram ya @official_mohamedhussein15 ameahidi kufanya vizuri mchezo wa marudiano jijini Cairo mbali na kupoteza kwa bao moja hapo jana dhidi ya Al Ahly ya Misri.

“Inshaallah tutarudi tukiwa imara zaidi na tutafanya vizuri game ya marudiano,” ameandika Zimbwe Jr.

Kupitia jukwaa hilo, Mohamed amewashukuru mashabiki wa Simba SC kwa ushirikiano waliouonesha.

“Jana mlijitokeza kwa wingi kutupa nguvu▲ #Nguvumoja,” ameandika Zimbwe.

Simba inataraji kusafiri Jumatano ya juma lijalo kwaajili ya mchezo wa marudiano wa hatua ya Robo Fainali, utakaochezwa Aprili 05, 2024 nchini Misri.

Habari Zifananazo

Back to top button