TSN, TISEZA kushirikiana kutangaza maeneo ya uwekezaji

DAR ES SALAAM; UJUMBE wa Menejimenti ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania (TSN), ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Asha Dachi, umekutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Gilead John Teri na maofisa wengine wa mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam leo Januari 9, 2025.

Taasisi hizo zimekubaliana kuboresha na kuendeleza ushirikiano katika kutangaza maeneo ya uwekezaji nchini.




