TSN, Xinhua kuimarisha ushirikiano

KAMPUNI ya Magazeti ya Serikali (TSN) imesema itaimarisha ushirikiano na Shirika la Habari la Xinhua la China.

Mkurugenzi Mtendaji wa TSN, Asha Dachi amesema hayo alipozungumza na ujumbe wa viongozi wa Xinhua katika makao makuu ya kampuni hiyo Dar es Salaam.

“Kupitia makubaliano yetu ya ushirikiano, TSN imepata heshima ya kutumia makala na taarifa kutoka Xinhua, shirika la habari linalotambulika duniani kwa utoaji wa taarifa sahihi,” alisema Dachi.

SOMA: TSN, Xinhua kuimarisha ushirikiano matumizi AI

Alisema fursa hiyo imeongeza wigo wa taarifa za kimataifa za TSN na kuwawezesha wasomaji kupata habari zilizochakatwa kwa uangalifu, zenye usawa na zinazotoka vyanzo mbalimbali, hususani kutoka China na maeneo mengine ya Asia.

Dachi alisema TSN na Xinhua wamekuwa na ushirikiano kwa muda mrefu uliochangia kujenga uelewa baina ya wananchi wa China na Tanzania.

Amesema ushirikiano huo umeimarisha upatikanaji wa habari za kimataifa zilizo sahihi na kuendeleza kubadilishana ujuzi wa kitaaluma kati ya waandishi wa habari wa Tanzania na China.

Alishukuru ubalozi wa China nchini kwa udhamini wake katika programu mbili za elimu za TSN kupitia majarida yake ya Elimika na Academy.

Jarida la TSN Academy huchapishwa kila wiki kwa Kiingereza kwenye gazeti la Daily News na Elimika huchapishwa kwa Kiswahili kwenye HabariLEO kila wiki.

Alisema majarida hayo yamekuwa majukwaa ya kushirikisha maarifa na kuendeleza dhamira ya TSN, Xinhua na ubalozi wa China katika elimu, ujenzi wa uwezo na maendeleo.

Dachi alisema TSN inapata msukumo wa kimaendeleo kutokana na ubobezi wa Xinhua katika matumizi ya teknolojia, uchambuzi wa takwimu na uandishi wa habari wa kisasa ili kukidhi mahitaji ya hadhira ya kisasa.

“Tunaamini bado yapo mambo mengi ya kujifunza kutoka Xinhua, hususani katika ubunifu wa kidijiti, uendeshaji wa chumba cha habari na uandishi wa kisasa,” alisema.

Mhariri Mkuu wa Xinhua, Lyu Yansong alisema shirika hilo litaendeleza ushirikiano huo uliopo baina ya kampuni hizo za habari ili kuendelea kuupatia ulimwengu habari na elimu kwa ujumla.

Lyu alisema wataimarisha upatikanaji wa habari sahihi za kimataifa na kuendeleza kubadilishana ujuzi wa kitaaluma kati ya Tanzania na China.

Habari Zifananazo

5 Comments

    1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
      .
      M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us →→→→→→→ https://Www.Work27.Online

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button