‘TTB tumieni AFCON 2027 kuongeza watalii’

DAR ES SALAAM: ILI kuhakikisha idadi ya watalii inaongezeka nchini na kufikia milioni nane kwa miaka mitano, Bodi ya Utalii Tanzania imetakiwa kutumia fursa ya Tanzania kuwa mwenyeji wa michuano ya Mataifa Afrika (AFCON 2027) ili kujitangaza zaidi na kuongeza idadi ya watalii nchini.
Agizo hilo limetolewa leo Novemba 26, 2025 na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji alipofanya ziara ya kikazi katika Bodi ya Utalii Tanzania jijini Dar es Salaam, huku akiitaka bodi hiyo kuongeza nguvu katika utafiti, kubadilisha mfumo unaotumika kuyafikia masoko ya bidhaa za utalii ili watalii waweze kuja nchini na kufikia lengo lililowekwa.
Pia ameisisitiza bodi hiyo kuboresha bidhaa wanazozipeleka sokoni, ikiwa ni pamoja na kutambulisha bidhaa mpya zinazopatikana nchini.

Dk. Kijaji amesema “Uwezo huo tunao kwasababu Taifa letu limebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii, na tumepeleka sokoni vichache sana. Kwa hiyo jukumu kubwa tulilowapa leo TTB ni kuhakikisha tunakuwa na bidhaa mbalimbali za utalii ambazo hatujawahi kuzifikisha sokoni ili watalii waliokuja awali waweze kurejea na wenzao wengine”
Aidha, ameielekeza bodi hiyo kuongeza nguvu kufanya utafiti ili kugundua vivutio ambavyo bado havijafika sokoni na kufahamu maeneo vinapopatikana, na ameitaka TTB kushirikiana na taasisi zinazomiliki vivutio hivyo.
“Angalau kwa kila mwaka tunakuwa na bidhaa mpya ya kupeleka sokoni, lengo lake ni nini?, na tuelewe kabisa soko lake ni lipi?, itawafaa watu wa aina gani, na lugha itakayotumika sokoni, na tuwe na mgawanyiko wa wateja ili kuwaleta hao watalii milioni nane.” Amesema Dk. Kijaji.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com