TTCL waja kivingine huduma intaneti

DAR ES SALAAM: Shirika la Mawasiliano Tanzania, (TTCL) limezindua huduma mpya ya intaneti yenye kasi ijulikanayo kama “Faiba Supersonic Experience.

Lengo ni kuwapatia Watanzania huduma bora, ya uhakika na gharama nafuu katika katika kukuza uchumi wa kidijitali.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika Machi 16, 2026, Mkurugenzi wa Biashara wa TTCL, Vedastus Mwita amesema huduma hiyo inalenga kuongeza kasi ya matumizi ya teknolojia.

Amesema kupitia huduma ya Faiba Mlangoni Kwako, wateja wataweza kufurahia intaneti yenye kasi kubwa itakayowawezesha kufanya shughuli nyingi za kidijitali kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa Vedastus Mwita, vifurushi vipya vya huduma hiyo vinakuja na kasi kuanzia 60 Mbps hadi 250 Mbps pamoja na ofa ya laini za simu za mkononi za TTCL bure kwa wateja watakaojiunga na vifurushi husika.

Amesema uzinduzi wa huduma hiyo ni sehemu ya juhudi za shirika hilo kuendelea kuimarisha miundombinu ya mawasiliano nchini na kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanapata intaneti ya uhakika kwa ajili ya kukuza uchumi wa kidijitali.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button