Tuendelee kuijenga nchi kwa umoja

“AMANI haina deni na Watanzania mmeelewa vizuri msemo huo tangu miaka ya 1960. Tanzania imeendelea kuwa mfano kwa umoja na amani. Kwa hiyo, kwa miaka mitano ijayo tunawatakia muendelee kuwa na amani, umoja na kushiriki maendeleo”.
Hiyo ni kauli ya Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye aliyotoa Novemba 3, 2025 wakati Rais Samia Suluhu Hassan akiapa. Inabeba uzito mkubwa na ujumbe wa kizalendo kwa Watanzania wote.
Huu ni mwito muhimu kutoka kwa kiongozi huyu wa nchi jirani ambayo pia ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaohimiza Tanzania kuendeleza misingi yake ya kuwa taifa lenye heshima kubwa barani Afrika.
Watanzania wamekuwa mfano wa kuigwa kwa kuishi kwa amani, kuheshimiana na kushirikiana bila kujali tofauti za dini, kabila, wala rangi.
SOMA: Umoja wa kitaifa utalinda amani ya nchi
Hii ndiyo misingi iliyowekwa na waasisi wa taifa letu, ikiongozwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Amani hii imekuwa nguzo ya maendeleo yetu na kichocheo kikubwa cha uchumi kukua, uwekezaji kustawi na huduma za kijamii kuboreshwa.
Ni kweli, amani haina deni na Watanzania wanaelewa vizuri msemo huo tangu miaka ya 1960, lakini inalindwa kwa vitendo na dhamira ya pamoja ya wananchi na viongozi wao.
Kauli ya Rais Ndayishimiye inapaswa kuwa chachu kwa Watanzania kutafakari wajibu wao katika kizazi cha sasa ambacho nchi imefika hatua ya kipekee ya ukuaji wa maendeleo chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa kinara wa diplomasia, umoja na mageuzi ya kiuchumi.
Hivyo, jukumu letu wananchi ni kuunga mkono juhudi hizi kwa kufanya kazi kwa bidii, kulinda amani na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Kila Mtanzania ana nafasi katika safari hii. Wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara, vijana na wazee; wote wanapaswa kuona wajibu wa kuchangia ustawi wa taifa wakitambua kwamba umoja wetu ni silaha muhimu ya kushinda changamoto za kiuchumi na kijamii.
Tukianza kugawanyika kwa misingi ya kisiasa au kikabila, tutakuwa tunahatarisha urithi wetu wa amani ambao dunia nzima inautambua.
Kwa hiyo, maneno ya hekima ya Rais Ndayishimiye hayana budi kuzingatiwa kwa vitendo na kila Mtanzania anaendeleza amani, umoja na kushiriki maendeleo. Lawama zisizo na tija, fitina na maneno ya kuchonganisha yasipewe nafasi.
Badala yake, tuungane kama Watanzania katika kuijenga Tanzania tunayoitaka, yenye uchumi imara, elimu, afya yenye ubora na heshima katika jumuiya ya kimataifa.
Watanzani tuungane kwa pamoja kuifanya Tanzania iendelee kuwa kisiwa cha amani na matumaini. Wito wetu kwa Watanzania wote ni kushikamana, kushiriki kulinda amani na kuimarisha ustawi wa nchi ili kukidhi matakwa ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Utekelezaji wa dira unalenga ustawi wa jamii katika kujaza pengo la kiuchumi kwenye ngazi ya kaya kupitia ongezeko la mapato ya serikali na mtu mmojammoja, kundeleza na kuimarisha rasilimaliwatu kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kijamii kwa kila Mtanzania.
Ili maendeleo hayo yatekelezwe kwa vitendo, ni jukumu la kila Mtanzania kuimarisha umoja na amani.




BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”
BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”
BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”
BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”
BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”