‘Tuenzi Muungano kwa kufanya kazi’

KATAVI; MKUU wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Onesmo Buswelu, amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kushikamana na kudumisha upendo, amani pamoja na kufanya kazi halali za maendeleo.

Amesema hayo katika mdahalo wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mpanda Ndogo, ambapo amesema ni vyema kuheshimu utulivu na amani ambayo inajengwa na Muungano uliopo.

Amesema kupitia Muungano, maendeleo mengi nchini yamepatikana ikiwemo ya kiuchumi, afya, elimu pamoja na uboreshaji miundombinu ya kijamii.

Advertisement

“Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius  Nyerere na hayati Abeid Amani Karume waliweka maisha yao nyuma, lakini wakaweka maslahi ya Watanzania mbele na ndiyo maana leo hii tunawaambia Watanzania umuhimu wa kuwa na Muungano na sisi tunaofuata nyuma yao tuna jukumu la kuulinda, kuutunza na kuudumisha,”amesema Buswelu.