Tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kudumisha amani, umoja wa kitaifa

JANA taifa liliadhimisha miaka 26 tangu kuondokewa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambaye alijijengea heshima kubwa ndani na nje ya mipaka ya nchi kwa misingi imara ya uongozi, utu, haki, usawa na amani aliyoiacha kama urithi wa kudumu kwa Watanzania.

Katika kila kumbukizi ya kifo chake, taifa hujikumbusha dhamira kuu ya Mwalimu Nyerere ya kuona Watanzania wakiishi kwa umoja, upendo na heshima bila kujali tofauti za dini, kabila au itikadi za kisiasa.

Msingi huo ndio umeifanya Tanzania kuwa ‘Kisiwa cha Amani’ barani Afrika.

Njia bora zaidi ya kumuenzi Mwalimu Nyerere haipaswi kuwa kwa maneno, bali kwa vitendo vinavyoendeleza misingi aliyoiamini.

Miongoni mwa misingi hiyo ni uadilifu katika uongozi, kuheshimu sheria, kulinda utu wa mwanadamu na kuhakikisha kila Mtanzania anapata haki zake za msingi.

Vilevile, ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda amani aliyoiacha kwa kuwa amani ndiyo nguzo kuu ya maendeleo ya taifa lolote.

Nchi inapoelekea kwenye kipindi cha Uchaguzi Mkuu,maadhimisho haya yanapaswa kuwa mwongozo wa kutafakari wajibu wetu wa kulinda misingi ya amani, umoja na utulivu.

Ni wakati wa viongozi wa kisiasa, wagombea, vyama pamoja na wananchi kwa ujumla kutanguliza uzalendo na busara kwa kauli na matendo.

Hawana budi kujiepusha na lugha za chuki, kejeli, uchochezi na propaganda zinazoweza kuibua migawanyiko isiyo ya lazima.

Tunahimiza taasisi za kiraia na wadau wote wa demokrasia kushirikiana kuhakikisha kuwa mchakato mzima wa uchaguzi unafanyika kwa amani, haki na uwazi.

Hayo ndiyo maono ambayo Mwalimu Nyerere aliyapigania kwa moyo wa dhati kwa kuhakikisha nchi inaendelea kuwa mfano wa demokrasia yenye nidhamu na utulivu Afrika na dunia nzima.

Kimataifa Tanzania imeendelea kuwa nembo ya diplomasia ya amani ikiwa imechangia kikamilifu katika juhudi za kutafuta suluhu ya migogoro katika nchi mbalimbali barani Afrika.

Hii ni heshima kubwa iliyojengwa kutokana na misingi ya uongozi wa Nyerere uliojielekeza katika ujirani mwema. Kwa msingi huo; viongozi, wananchi na taasisi mbalimbali nchini zinapaswa kuwa walinzi wa urithi huu wa thamani.

Kila mmoja atambue kwamba kumuenzi Mwalimu Nyerere ni kuishi kwa misingi ya haki, utu na amani kwa kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa taifa lenye mshikamano na dira ya maendeleo endelevu.

Habari Zifananazo

4 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

    1. Earn cash with a job that lets you make more than $700 per day. Get paid weekly with earnings of $3,500 or more by simply doing easy online work. No special skills are required, and the regular earnings are amazing. All you need is just 2 hours a day for this job, and the income is fantastic. Anyone can get started by following the details here:

      COPY THIS →→→→ http://Www.Work99.Site

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  3. I get paid more than $100 to $500 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this I have earned easily 💵$20k from this without having online working skills . Simply give it a shot on the accompanying site…

    Here is I started.→→→→→→→→→ https://Www.Works6.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button