Tunduru watakiwa kupanda miti maeneo yao

Tunduru watakiwa kupanda miti maeneo yao

MKUU wa Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, Julius Mtatiro amewataka viongozi ngazi ya vijiji, kata na halmshauri kuhakikisha upandaji miti inakuwa ni suala endelevu katika maeneo yao ya usimamizi, ili kusaidia uhifadhi mazingira.

Mtatiro ametoa maagizo hayo leo baada ya kuongoza upandaji miti katika eneo la Kanisa la Upendo la Kristo Masihi (KIUMA), Kata ya Matemanga Wilaya ya Tunduru.

Amewataka viongozi wa ngazi hizo kuhamasisha wananchi kupanda miti kwenye maeneo yao na kuwaelekeza aina ya miti inayofaa na haileti athari kwenye mazingira, hasa kwenye vyanzo vya maji.

Advertisement

Amesema uharibifu wa mazingira unaongezeka wilayani humo kutokana na shughuli za kibinadamu, ikiwemo kilimo na ufungaji holela, huku akilaumu wahusika kushindwa kupanda miti mipya, ili kuzuia athari za kimazingira, ambazo zinahatarisha maisha ya binadamu na viumbe hai wengine.

“Suala la upandaji miti ni muhimu katika jamii yetu, kwani linasadia kukabiliana na changamoto ya hewa ukaa, inayoweza kuhatarisha maisha ya binadamu, hivyo wananchi wana wajibu wa kuzuia athari kwa kupanda miti mipya kila mara,” amesema.

Katibu wa taasisi ya KIUMA,  Daniel Malukuta amesema taasisi hiyo imeweka utaratibu wa kuotesha miche na kupanda miti kuzunguka maeneo ya taasisi hiyo kutunza mazingira.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *