Tusihofu: Bado mbili za mwisho

Stars wapo kamili kuiua Uganda

*Tusubiri mechi mbili za mwisho*

IMEBAKI michezo miwili kufahamu mustakabali wa Tanzania katika kundi F, baada ya leo kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Morocco.

Katika mchezo huo uliopigwa muda mchache uliopita uwanja wa Laurent Pokou San Pedro, Stars imepoteza mabao 3-0.

Advertisement

Mabao ya Morocco yamefungwa na Roman Saiss, Azzedine Ounahi na Youssef En-Nesyri.
Stars sasa itasubiri mchezo unaofuata dhidi ya Zambia utakaochezwa Januari 21, 2024 katika uwanja huo.

Mchezo wa mwisho wa kumaliza hatua ya makundi, Tanzania itakutana na DR Congo Januari 24.

Ili kufufua matumaini ya kusonga 16 bora, Stars inapaswa kushinda mchezo unaofuata dhidi ya zambia.