Tutafungia leseni – Polisi

Yaonya sheria hazijabadilika

DODOMA: JESHI la Polisi nchini limewaonya madereve kuwa litawafungia leseni wote wanaosababisha ajali.

Onyo hilo limekuja ikiwa siku za karibuni kuwa na matukio mengi ya ajali za barabarani zilizosababisha vifo na majeruhi kwa watanzania.

Kwa mujibu wa taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP, David Misime imesema uchunguzi uliofanyika unaonyesha kuwa chanzo cha ajali nyingi ni uzembe wa madereva wanaoendesha magari hayo.

Misime amesema mbali na uzembe pia ni mwendo kasi na kupita magari mengine (overtake) bila kuchukua tahadhari maeneo ambayo alama za barabarani zimekataza.

Amesema, pamoja na uzembe huo unaofanywa na baadhi ya madereva, wa magari hayo kumekuwa na maneno ya kuiaminisha jamii kuwa mwisho wa mwaka ajali zinakuwa nyingi, jambo ambalo si sahihi huku akiwataka madereva kuondoa dhana hiyo ambayo inapotosha umma wa Tanzania.

“Kinachobadilika ni tabia za baadhi ya madereva wa vyombo vya moto wasiotaka kuzingatia sheria za usalama barabarani na kufuata alama za makatazo na zile za ishara za barabarani na matokeo yake wanasababisha ajali,”amesema na kuongeza

“Mwisho wa mwaka hakujabadili sheria za usalama barabarani wala alama za makatazo na ishara za barabarani, madereva wafuate sheria ili kuepuka ajali za barabarani,”amesisitiza.

Misime amewataka watumiaji wa barabara wakiwemo watembea kwa miguu, wasukuma mikokoteni, waendesha baiskeli na waendesha vyombo vya moto wazingatie sheria za usalama barabarani huku akiwaomba viongozi wa serikali kuwaonya madereva wao pale wanapokiuka sheria za usalama barabarani.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button