‘Tutahakikisha amani, mshikamano vinadumu’

ZANZIBAR; Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Hemed Suleiman Abdulla, amesema serikali itaendelea kuhakikisha amani na mshikamano uliopo nchini unadumu na kuimarika zaidi.

Amesema hayo wakati wa ufunguzi wa kongamano la kuhamasisha amani kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 lililofanyika katika ukumbi wa Umoja ni Nguvu, kisiwani Pemba.

Amesema amani na mshikamano ndio nyenzo muhimu ya kuleta maendeleo na bila ya amani hakuna maendeleo yatakayofikiwa na badala yake ni uharibufu wa miundombinu na watu kupoteza maisha yao na mali zao.

Amesema mafanikio makubwa yaliyopatikana Zanzibar na Tanzania kwa ujumla ikiwemo uimarishaji wa sekta elimu, afya, barabara, maji safi na salama, bandari, masoko na uimarishaji wa maslahi ya wafanyakazi, yamesaindia kwa kiasi kikubwa kuongeza ustawi wa wananchi.

Ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya siasa kuhakikisha wakati wote wanatumia kauli zitakazodumisha umoja na mshikamano na sio kuchochea, kuwagawa watu na kuvuruga amani.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button