Tuzo kiungo bora sio inshu kwa Chama

KUINGO wa Simba, Clatous Chama amesema sio jambo kubwa kwake kutajwa kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya kiungo bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Chama anasema jambo kubwa kwake ni watu kuona anachokifanya Simba, hivyo furaha yake ni kuisaidia timu yake kufikia malengo iliyojiwekea kwa msimu husika.

Kuhusu kivumbi cha kumtafuta kiungo bora, Chama amesema amekoshwa na kiwango kilichooneshwa na viungo wenzake wa Simba, Saido Ntibazonkiza na Mzamiru Yassin na kuwatakia kila lenye kheri katika kinyan’ganyiro cha kuwania tuzo hiyo.

“Kwakweli msimu ulikuwa mzuri sana kwetu sisi watatu, kila mmoja amefanya vizuri sana, na amejitahidi kuisadia timu, yoyote atakaeshinda tuzo hii nitakuwa na furaha.” Alisema Chama

Wachezaji wengine wanaowania tuzo hiyo ya kiungo bora ni Bruno Gomes wa Singida Big Stars na Stephan Aziz Ki wa Yanga.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button