Ubunifu wazidi kupaa chuo cha Nyerere

Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kimeendelea kuonyesha umahiri wa bunifu mbalimbali ikiwemo kituo atamizi kwaajili ya kuendeleza bunifu kwakushirikiana na taasisi nyingine ili ziweze kuingia sokoni na kuzalisha ajira kwa vijana.

Akiongea katika Maonyesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi(NACTVET) , Mkuu wa Chuo hicho,Profesa Shadrack Mwakalila amesema chuo hicho kinatoa mchango mkubwa kwa taifa ikiwemo utoaji wa maarifa kwa vijana ili waweze kujiajiri.

Alisema bunifu za wabunifu zikiingia sokoni zitazalisha ajira kwani chuo hicho kinawanafunzi wanaofanya bunifu mbalimbali hususan katika mfumo wa umwagiliaji usiohitaji mkulima kukaa shambani ikiwemo mfumo wa kusaidia kufukuza ndege wakiingia shambani lakini pia kunaubifu wa kifaa maalum kinachowekwa katika banda la kuku kwaajili ya kudhibiti wizi wa kuku.

“Tutashirikiana na taasisi za fedha ili kuwezesha bunifu zinazozalishwa ziwe na tija na kuzalisha ajira zaidi lakini pia kunaubifu ya kudhibiti wizi wa kuku kwenye mabanda”

Naye mbunifu aliyetengeneza banda la kuku kwa kuweka kifaa maalum kinachopiga kelele ili kumtarifu mwenye kuku kunawizi,Nauriya Salim Abdallah anayesoma chuo cha Mwalimu Nyerere amesema ameamua kuonyesha bunifu hiyo kwaajili ya kudhibiti wizi wa kuku unaotokea kwa wafugaji hivyo alitoa rai kwa wafugaji kutumia tenkolojia hiyo inayopatikana katika chuo hicho ili waweze kufuga na kupata manufaa zaidi.

Habari Zifananazo

Back to top button