Uchumi wapaa, pato lakua Z’bar

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema mafanikio yaliyopatikana visiwani humo katika miaka 61 sasa yametokana na Mapinduzi ya Zanzibar, jitihada za wananchi na viongozi wa awamu zote zilizotangulia.
Hivyo dhamira ya serikali ya sasa ni kuendelea kudumi sha malengo ya mapinduzi kwa kuleta mageuzi ya kiuchumi ili kuongeza kasi ya maendeleo na ustawi wa maisha ya wananchi wa Zanzibar.
Dk Mwinyi alisema hayo jana kwenye hotuba yake ka tika Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
“Mapinduzi ya mwaka 1964 ni tukio muhimu la historia ya nchi yetu, waasisi wa taifa letu wakiongozwa na jemedari wa Mapinduzi, Mzee Abeid Amani Karume walijitoa mhanga kuikomboa nchi na kufungua ukurasa mpya wa maendeleo,” alisema Dk Mwinyi.
Alisema wakati akizindua Baraza la Wawakilishi mwa ka 2020, alibainisha dhamira ya serikali kudumisha malengo ya mapinduzi kwa kuleta mageuzi ya kiuchumi ili kuongeza kasi ya maende leo na ustawi wa maisha ya wananchi wa Zanzibar.
Alisema serikali ya sasa ambayo imeingia madarakani miaka minne iliyopita, ime fanya juhudi za kuendeleza mafanikio yaliopatikana na kuhakikisha Zanzibar inazidi kupiga hatua za maendeleo katika sekta zote pamoja na kudumisha misingi ya amani, uzalendo na umoja wa kitaifa.
Alisema dhamira hiyo inaendelea kutimizwa kwani uchumi wa Zanzibar umeendelea kuimarika na hadi kufikia Septemba 2024, ulifika asilimia 7.5.
Aidha, alisema pato la taifa kwa bei ya soko (GDP) limeongezeka kufikia thamani ya Sh trilioni 6.04 mwaka 2023 kutoka Sh tri lioni 4.78 mwaka 2021 am bayo ni sawa na ongezeko la asilimia 26.
Akizungumzia kuongezeka kwa pato la taifa na ukuaji wa uchumi, Dk Mwinyi alisema kumesa babishwa na kuimarika kwa sekta ya huduma iliyokuwa kwa wastani wa asilimia 9.9 mwaka 2023 kutoka wastani wa asilimia 1.3 mwaka 2021.
Aidha, alisema sekta ndogo ya huduma za watalii imeimarika kwani idadi ya watalii wanaotem belea Zanzibar imeongezeka kwa asilimia 145 katika kipindi hicho.
“Si ongezeko la watalii pekee, kadhalika, tume ongeza ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa asil imia 51 kutoka Shilingi bil ioni 858.2 mwaka 2020/2021 hadi kufikia shilingi trilioni 1.3 mwaka 2022/2023,” alisema.
Alisema mfumuko wa bei umeendelea kudhibitiwa na kubaki katika tarakimu moja na kuwa kwa upande wa Zanzibar ulipungua hadi kufika asilimia 4.5 Novemba, 2024.
Akizungumzia mafanikio ya uwekezaji, Dk Mwinyi alisema yametokana na jitihada za kuvutia wawekezaji na kuwa miradi 449 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 5.9 imesajiliwa na Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar.
Alisema miradi hiyo inatarajiwa kuzalisha ajira zaidi ya 22,966 na miradi hiyo ni ya uwekezaji kwe nye sekta ya hoteli yenye miradi 169, biashara za majengo miradi 99, viwanda miradi 43, kilimo miradi 28, michezo miradi 28 na sekta nyingine zenye miradi 82.
Katika sekta ya viwanda, Dk Mwinyi alisema wamepata mafanikio kwa kuimarisha miundombinu ya barabara, umeme na hu duma za maji safi na salama katika maeneo yanayoleng wa kuanzishwa viwanda.
“Shilingi bilioni 33.12 zimetumika kwa ujenzi wa miundombinu katika eneo la Dunga Zuze, tumefani kiwa kuvutia wawekezaji na tumeshatoa hati za ukodishaji wa ardhi kwa wawekezaji saba,” alisema.