Uchunguzi kuwabaini wang’oa viti Lupaso

TANGA: NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘mwanafa’ amekemea vitendo vya uharibifu wa miundombinu ya Uwanja wa Benjamini Mkapa ikiwemo kung’olewa kwa viti vya uwanja huo na kusema vitendo hivyo ni vya kihuni.

Akiwa jijini Tanga katika tukio la uzinduzi wa ligi ya Odo Ummy CUP katika Jimbo la Tanga mjini, Mwanafa amesema Serikali inafanya uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na vitendo hivyo ili kuchukuliwa hatua.

Kupitia mitandao ya kijamii kuna video zikionesha vitendo viovu vya uharibifu wa miundombinu ya uwanja unaohusishwa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kati ya Yanga na Al Ahly uliomalizika kwa sare ya 1-1 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam, Desemba 02, 2023.

“Tunafanya uchunguzi, ukikamilika, miongoni mwa taarifa zitakazokuja ni za gharama za uharibifu ule na wahusika watalipia tu,” amesema Mwinjuma akirejea tukio la mwaka 2016 kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Yanga Uwanja wa Benjamini Mkapa.

“Ni kweli nimeliona, ule ni uhuni kama uhuni mwingine.

Kama ambavyo viti viliwahi kung’olewa na watu wakalilipishwa kufanya ukarabati ule, hakuna kitu kitakachobadilika.” Amesema kiongozi huyo.

Habari Zifananazo

Back to top button