UHOLANZI : MWENDESHA mashtaka wa ICC Karim Khan amesema ataanzisha upya uchunguzi wa madai ya uhalifu uliofanyika tangu mwaka 2022, katika jimbo linalokumbwa na migogoro mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari Khan amesema ghasia za hivi karibuni zianzoendelea katika jimbo la Kivu ya Kaskazini zinahusiana na mifumo ya vurugu na uhasama ambao umelikumba eneo hilo tangu katikati ya mwaka 2002.
ICC ilianzisha uchunguzi kwa mara ya kwanza nchini Kongo miaka 20 iliyopita, kufuatia miaka mingi ya vita vya makundi ya wapiganaji wenye silaha.
Mwaka uliopita, serikali ya Kongo iliiomba ICC kuchunguza madai ya uhalifu huko Kivu ya Kaskazini uliofanywa na makundi yenye silaha yanayoendesha shughuli zake tangu Januari 1, 2022.