UDOM watafiti tiba upungufu wa damu

DAR ES SALAAM; CHUO Kikuu cha Dodoma ( UDOM), kimetafiti bidhaa iliyoandaliwa kwa kutumia chakula na matunda inayotibu upungufu wa damu unaotokana na upungufu wa madini chuma mwilini.

Pia bidhaa hiyo inatibu maambukizi ya bakteria katika mfumo wa utoaji taka.

Mwanafunzi wa Shahada ya Tiba chakula na lishe chuoni hapo, Mussa Kasela amesema hayo wakati wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ‘Sabasaba’ yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

” Bidhaa hizo tumeandaa katika mfumo wa poda ambayo matumizi ni kama inavyokuwa kwenye juisi.

“Anachukua glasi anaweka kijiko kimoja cha chai ndani ya hayo maji, anakoroga anakunywa mara moja kwa siku, kwa muda wa siku10 hadi 14,” amesema.

Ameshauri kabla mtumiaji hajaanza kutumia awe na vipimo vinavyoashiria ana matatizo hayo.

 

Habari Zifananazo

Back to top button