Ufaransa, Tanzania kushirikiana kilimo ikolojia

MOROGORO: SERIKALI ya Ufaransa itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kilimo ikolojia kinachohifadhi ardhi na mazingira kwa lengo la kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa uhakika wa usalama wa chakula kitakachosaidia soko la ndani ya nchi na nyingine jirani.
Balozi wa Ufaransa hapa nchini, Anne Sophie Ave amesema hayo mjini Morogoro kwenye uzinduzi mradi wa AgroKilimo unatekelezwa na Shiriki la Kimataifa lisilo la Kiserikali la Islands of Peace Tanzania.
Mradi wa AgroKilimo wa miaka miwili na umeanza kutekelezwa mwaka 2025 na utafikia ukomo mwaka 2027 ambao Serikali ya Ufaransa imetoa zaidi ya Sh Bilioni 1.4.
Balozi wa Ufaransa nchini amesema mradi huo utasaidia kuongeza uzalishaji wa matunda na mbogamboga ambazo hazitumii kemikali kwa faida za nchi hizo mbili.
Amesema kwa miaka mingi Tanzania na Ufaransa zimekuwa zikishirikiana kwenye sekta kilimo na kutole mfano wa ujenzi wa soko la Nyandira lililopo wilaya ya Mvomero ambalo lina miaka zaidi ya 30 likuwasaidia wakulima kupata masoko ya mazao yao.
Amesema nchi yake inajivunia kuwa na miradi mingi ya sekta ya kilimo katika mikoa mbalimbali hapa nchini,ikiwemo kilimo cha Ikolojia sehemu za milimani, uzalishaji kutoka kwenye mbegu hadi chakula na ujenzi wa masoko mbalimbali hapa nchini yanayowasaidia wakulima.
Balozi wa nchi hiyo amesema mradi huo unalenga pia kuviimarisha na kuvijengea uwezo vituo sita vya mafunzo ya kilimo ikolojia vilivyotapakana katika maeneo mbalimbali nchini ili viweze kuwa na ushirikiano wa pamoja kusaidia wakulima watumie mbinu rafiki za uzashaji na kutunza mazingira yanayowazunguka.
“Tunataka kuona kilimo kinaleta chakula,ajira na kuchangia maisha ya wakulima ili wakihifadhi mazingira na kuifanya Dunia kuwa salama na endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo,” amesema Balozi wa Ufaransa Anne.
Naye Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kibelgiji la Islands of Peace Tanzania, Ayesiga Buberwa amesema Mradi wa AgroKilimo, unatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili kwa kushirikiana na vituo sita vya mafunzo ya kilimo ikolojia vilivyo katika maeneo mbalimbali nchini.
Buberwa amesema mradi huo utasaidia kuongeza nguvu kwenye mifumo endelevu ya chakula kwa kupitia kilimo Ikolojia na utasaidia kufundisha wawezeshaji ili na wao wakafundishe wakulima vijijini.
Amesema mradi huo utafanya tafiti shirikishi moja kwa moja na wakulima ili kuweza kuwafikishia teknolojia za kilimo ikolojia, kutatua changamoto zinazowakabili ili wapate majawabu ya kusaidia kuongeza uzalishaji.
Buberwa amesema kwa kushirikiana na Serikali ya Ufaransa waliweza kupata mradi wa kuvisaidia vituo hivyo vya mafunzo ya kilimo ili viweze kuwa na mfumo wa pamoja wa kufundishia wakulima teknolojia ya kilimo cha Ikolojia zinasambaa kote nchini.
Amesema mradi huo utakuwa unasaidia vituo hivyo kulingana na mahitaji yao ikiwemo sehemu ya kuoneshea, miundombinu, elimu kwa watendakazi kwenye vituo ikiwa na kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).
Buberwa amesema kwa Chuo Kikuu hicho kupitia Kitivo cha Kilimo Ikolojia, mradi huo utawasaidia wanafunzi wanaosoma shahada ya pili ya kilimo ikolojia kwenda kufanya tafiti mbalimbali kwa wakulima zitakozosaidia kutatua changamoto kuhusu kilimo ikolojia.
Naye Ofisa Kilimo wa Shirika la Islands of Peace ,Emmanuel Kasembe, amesema Kilimo Ikolojia kinazingatia uhifadhi wa ardhi , mazingira na viumbe muhimu waliozunguka.
Kasembe amesema tunaposisitiza kutumia kilimo ikolojia kinampa mkulima nafasi ya kuwa na uwezo wa kuchanganya mazao zaidi moja shambani kwake.
“….kilimo hiki kinamuelekeza namna gani anaweza kupanda kwa eneo dogo na kuzalisha kwa wingi mazao tofauti huku akirutubisha udongo kwa matumizi ya baadae” amesema Kasembe.
Are You Responsible For Leaves From Your Neighbor’s Tree?
What to do when the leaf cleanup falls to you.
By Brandee Gruener Published on September 30, 2025
In This Article
Who Is Responsible?
Throwing Leaves Back
What To Do With Leaves
Keep Leaves Off Your Property
A huge pile of raked fallen autumn leaves in a yard.