Ugonjwa wa sikoseli unavyotesa watoto Shinyanga

SELIMUNDU sikoseli ni ugonjwa wa kurithi ambao hutokea baada ya mwili wa binadamu kuwa na upungufu katika umbile la seli hai nyekundu za damu.

Wataalamu wa afya wanabainisha mgonjwa mwenye upungufu huo anakuwa na sikoseli haonyeshi dalili yoyote mpaka mtoto afikishe miezi minne ya umri tangu kuzaliwa na huanza na dalili mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika mwili wake.

Baadhi ya wazazi kutoka kijiji cha Nyasamba wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wanaeleza wanavyoteseka na watoto wenye ugonjwa wa sikoseli ambao unawafanya kudumaa kutokana na hali duni ya kipato ndani ya familia namna yakuukabilia ugonjwa huo.

Advertisement

Seni Mwinamila mkazi wa kijiji cha Nyasamba kata ya Bubiki Halmashauri ya Wilaya Kishapu anasema ugonjwa wa sikoseli umefanya watoto wake wawili kupoteza maisha na mwingine mwenye miaka mitatu anaendelea kusumbuka na ugonjwa huo.

Mwinamila anasema alikuwa akimpeleka kwenye zahanati lakini alipatiwa rufaa ya kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na aligundua kuwa mwanaye ni mgonjwa wa sikoseli akashauriwa na daktari kila mwisho wa mwezi ampeleke kliniki na sasa anaendelea na matibabu.

Mwinamila anasema changamoto ya kulea mtoto mwenye sikoseli ni kazi ngumu kutokana na hali duni ya maisha maana dalili zake muda mwingine zinakuja kwa kushtukiza na pesa ya usafiri ni shida,

Mwinamila anasema mtoto wake mwenye umri wa miaka mitatu amekuwa akiishiwa damu mara kwa mara nakuongezewa wakati mwingine uzito wa mwili kupungua na kutokwa manjano.

“Ugonjwa huu unahitaji mtu awe na pesa muda wote maana dalili zinakuja kwa kushtukiza pia chakula bora apate kwa kawaida ninampatia matunda na mboga za majani ili asipungukiwe damu lakini tatizo linakuwa palepale.”anasema Mwinamila.

Shanila Fale mkazi wa kijiji cha Nyasamba anasema amebahatika kupata watoto wanane wawili walifariki kwa nyakati tofauti wakiwa na umri chini ya miaka mitano kwa ugonjwa wa sikoseli na mmoja mwenye miaka mitatu sasa naye anatatizo la sikoseli ameonekana kudumaa.

“Nimekuwa nikienda hospitalini mara kwa mara wanampatia dawa lakini tatizo bado linakuwa la kuishiwa damu anaiomba serikali isaidie watoto wenye matatizo kama haya wapate msaada wa chakula chenye lishe.”anasema Fale.

Mtendaji wa kijiji cha Nyasamba, Speratus Rwehumbiza anasema watoto waliobainika na sikoseli wanatambulika katika ofisi yake ila wazazi wengine wamekuwa wakionekana kushindwa kumudu hali za watoto wao sababu ya kifedha huja kuomba msaada na wengine kukimbilia kwa waganga wa kienyeji..

Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Marwa Ngutuyi anasema sikoseli imekuwa ni tatizo kwa watoto ambao imewafanya kupungukiwa na damu na kulazwa mara kwa mara.

Dk Ngutuyi anasema ugonjwa huo unatokana na vinasaba yaani kurithi na Kanda ya Ziwa imekuwa ikiongoza kwa watoto wenye sikoseli ikiwemo Mkoa wa Shinyanga ambapo inalazimika kuanzisha kliniki ya watoto hao kwaajili ya wazazi kuwapa ushauri ili kupunguza tatizo la kulazwa kila mara.

Dk Ngutuyi anasema kuna watoto zaidi ya 100 wanaohudhuria kliniki mpaka sasa ikiwa ugonjwa wa sikoseli una sehemu mbili kuna watoto wanao onyesha kuwa na dalili na wengine wanakuwa na chembechembe au vimelea.

“Ugonjwa wa sikoseli unapona kama ukifuata utaratibu unaoelekezwa na wataalamu ila wanapokuwa wakubwa bado kuna mifupa itakayo kuwa imelika nakuonekama akiwa anatembea kuchechemea na mwili kuwa dhaifu”anasema Dk Ngutuyi.

Anasema mtoto kuanzia umri wa miaka 0 hadi mitano akiugua muda mrefu bila kupata matibabu ni hatari kwani hata ubongo wake unakuwa haufanyi kazi vizuri ni vyema wazazi wakawa wanachukua tahadhari mapema pindi wanavyoona dalili zozote mbaya kwa watoto wao.

Dk Ngutuyi anasema ugonjwa huo unatokana na vinasaba yaani kurithi na kanda ya ziwa imekuwa ikiongoza kwa watoto wenye sikoseli ikiwemo Mkoa wa Shinyanga ambapo inalazimika kuanzisha kliniki ya watoto hao kwaajili ya wazazi kuwapa ushauri ili kupunguza tatizo la kulazwa kila mara.

Anasema kuna watoto zaidi ya 100 wanaohudhuria kliniki mpaka sasa ikiwa ugonjwa wa sikoseli una sehemu mbili kuna watoto wanao onyesha kuwa na dalili na wengine wanakuwa na chembechembe au vimelea.

“Ugonjwa wa sikoseli unapona kama ukifuata utaratibu unaoelekezwa na wataalamu ila wanapokuwa wakubwa bado kuna mifupa itakayo kuwa imelika nakuonekama akiwa anatembea kuchechemea na mwili kuwa dhaifu”anasema Dk Ngutuyi.

Anasema mtoto kuanzia umri wa miaka 0 hadi mitano akiugua muda mrefu bila kupata matibabu ni hatari kwani hata ubongo wake unakuwa haufanyi kazi vizuri ni vyema wazazi wakawa wanachukua tahadhari mapema pindi wanavyoona dalili zozote mbaya kwa watoto wao.

Anaongeza kuwa ugonjwa wa sikoseli upo zaidi maeneo ya kanda ya ziwa kwani unatokana na vinasaba pia ugonjwa huu utakuta mtoto analazwa mara 15 kwa mwaka na afya yake inaonekana kuwa dhaifu.

Dk Ngutuyi anasema serikali kupitia Wizara ya Afya tayari imeleta vifaa vya utambuzi wa selimundu kwa watoto pindi wanapozaliwa lengo la kupambana na ugonjwa huo.

Dk Emmanuela Ambrose ambaye ni daktari bingwa wa watoto – kitengo cha damu Bugando jijini Mwanza anasema tatizo la ugonjwa wa sikoseli kuonekana kubwa jamii imekosa uelewa.

Ambrose anasema katika tafiti za hivi karibuni zinaonyesha katika Kanda ya Ziwa asilimia 21 ya watu wanarithi chembechembe (vimelea) za sikoseli .

Anasema tabia ya wazazi kuwaficha watoto wenye matatizo ya sikoseli wakihusisha tatizo hilo na imani za kishirikina ambayo inasababisha kuwaleta watoto hospitali wakiwa wamechelewa na kusababisha matatizo makubwa.

Dk Ambrose anasema ugonjwa huu hurithiwa kutoka kwa wazazi wote yaani baba na mama kitaalamu wanaita carriers.. mama na baba wanaweza kua hawana dalili yeyote lakini wamebebea vimelea vya ugonjwa huo kwenye damu zao na kumzaa mtoto mgonjwa.

Kwa mujibu wa Shirikia la Utangazaji la Uingereza (BBC) kupitia taarifa waliyoripoti mwaka 2015 wanaeleza kuwa Tanzania ni nchi ya tano kuwa na watu wenye ugonjwa wa sikoseli.

Ambapo wameleza utafiti unaonyesha kwa kila mwaka nchini Tanzania takribani watoto 1100 wanazaliwa wakiwa na sikoseli na moja ya sababu ya ongezeko hilo ni uelewa mdogo wa jamii juu ya ugonjwa huo unaosababisha seli za damu kuwa katika umbo la nusu duara.

Pia Taasisi ya Sikoseli nchini Tanzania mwaka 2014 nayo ilieleza kuwa watoto 800 hadi 1100 huzaliwa na sikoseli kila mwaka ikiwa ni nchi ya nne duniani kwa wagonjwa wenye sikoseli.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewataka vijana nchini kupima vinasaba na wenza wao kabla ya kuoana na kupata watoto ama kuanzisha familia ili kuvunja mnyororo wa maambukizi ya ugonjwa wa Selimundu,

Sheria ya mtoto ya mwaka 2009 namba 21 inaeleza wazazi na walezi wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha kwamba watoto wanapelekwa kwenye chanjo, wanapatiwa huduma za afya na kupewa miongozo au ushauri katika matunzo.

Sera ya afya ya mwaka 2007 nchini Tanzania linaeleza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaimarisha utoaji wa elimu ya afya ili kuhamasisha na kumwezesha kila mtu kujenga tabia inayozingatia kanuni za afya na maisha bora.

 

Imeandaliwa na Kareny Masasi

Tembelea //epaper.tsn.go.tz kusoma zaidi.

una maoni usisite kutuandikia

1 comments

Comments are closed.