Ujenzi SGR Tanzania, Burundi ni ukombozi EAC

SERIKALI ya Tanzania na ya Burundi zimeunganisha nguvu na kuzindua ujenzi wa mradi mkubwa wa kuunganisha miundombinu ya Reli ya Kisasa (SGR).

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye aliungana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuzindua ujenzi wa mradi huo katika hafla iliyofanyika Musongati, nchini Burundi mwishoni mwa wiki.

Majaliwa ambaye alimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan, alisema nchi hizo zimeweka msingi imara wa uhusiano kwa kutekeleza mradi unaounganisha nchi hizo na kuimarisha usafiri na usafirishaji wa kisasa.

Tunazipongeza nchi zote mbili kwa kufanikisha mradi huu muhimu kwa uchumi wa nchi hizo na wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa ujumla kwani ni wa kwanza kutekelezwa katika ukanda ukilenga kuimarisha na kupanua miundombinu ya usafirirshaji, kupunguza gharama na kuongeza ufanisi katika shughuli za kibiashara.

Juhudi za utekelezaji wa mradi huu wenye urefu wa kilometa 300, ikiwemo 240 za njia kuu na 60 za njia za kupishania pamoja na stesheni za kupakia abiria na mizigo, zinastahili kuthaminiwa na kuenziwa kwa manufaa ya EAC.

Tunaamini kuwa ujenzi wa reli hiyo utakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya viwanda, sekta ya kilimo, madini na sekta nyingine za uzalishaji kwa kutoa huduma ya usafiri wa uhakika kwa wananchi na wafanyabiashara kwenda Burundi.

Ni wazi kwamba utekelezaji wa mradi huu utarahisisha usafirishaji wa bidhaa ikiwemo madini ya nikeli.

Utachochea uhusiano, biashara na kufungua fursa zaidi kiuchumi si tu kwa Tanzania na Burundi, bali nchi nyingine za EAC.

Mafanikio mengine ya mradi huo ni pamoja na kupunguza muda wa usafirishaji na gharama ya kusafirisha mizigo kutoka Dar es Salaam hadi Bujumbura kwa asilimia 40.

Hima, wananchi wakiwemo wafanyabiashara pamoja na wawekezaji, tuiunge mkono Serikali ya Tanzania na Burundi kwa kuamua kwa dhati kutekeleza mradi huu ili kuhakikisha haukwami bali unakamilika kama ilivyopangwa kwa manufaa ya EAC.

Tunaamini uzinduzi wa ujenzi wa reli hiyo ya kisasa kati ya Burundi na Tanzania, ni hatua kubwa ya mwendelezo wa ujenzi hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa lengo la kuzidi kufungua ukanda mzima wa EAC kwa njia ya reli.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I make over thirty k a month working part-time. I kept hearing from other people telling me how much money they could make online, so I decided to find out. Well, it was all true and it completely changed my life.

    This Is Where I Started……….www.get.money63.com

  2. I make over thirty k a month working part-time. I kept hearing from other people telling me how much money they could make online, so I decided to find out. Well, it was all true and it completely changed my life.

    This Is Where I Started………. W­­w­­w­­.­­C­­a­­r­­t­­B­­l­­i­­n­­k­­s­.C­­o­­m

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button