Ujenzi wodi za VIP Muhimbili umesimama -CAG

DODOMA — Mradi wa ujenzi wa wodi za watu mashuhuri na binafsi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wenye thamani ya Sh bilioni 1.36, umesitishwa rasmi tangu Desemba 2023 kutokana na ukosefu wa fedha.

Mradi huo ulipaswa kukamilika ndani ya miezi sita lakini ulisimama kabla ya kukamilika, huku Hospitali ikisitisha mkataba wa mkandarasi Februari 2024.

Ripoti ya CAG kwa mwaka wa fedha 2023/24 imebaini kuwa idhini ya kutafuta wawekezaji ilitolewa na Wizara ya Afya, lakini kuanza mradi bila fedha ni kinyume na kanuni za manunuzi ya umma.

Kuna hatari ya kupotea kwa Sh milioni 71.51 zilizolipwa awali, huku dhamana ya malipo hayo ikiwa imekwisha muda wake. CAG amependekeza Hospitali ya Muhimbili ihakikishe upatikanaji wa fedha kabla ya kuanza miradi yoyote, pamoja na kuweka mifumo imara ya usimamizi wa kifedha na utekelezaji.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button