Ukarabati uwanja wa ndege Mtwara wafikia asilimia 96

Meneje wa kiwanja cha ndege mkoani Mtwara, Samuel Mruma amesema kuwa ukarabati kwa sasa upo hatua za mwisho za kumalizia kazi mbalimbali ikiwemo usindikaji wa taa za kuongozea ndege ili kuwezesha kufanya kazi masaa 24 ambapo kwa sasa kiwanja hicho kinafanya kazi kwa masaa 12 tu.

Amesema serikali ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 56.7 Kwa ajili ya upanuzi na ukarabati wa miundombinu ya kiwanja hicho ili kukipa hadhi ya kimataifa.

Upanuzi huo ulihusisha upanuzi wa njia za kurukia na kutua ndege (runaways), ujenzi wa njia za maungio, eneo la maegesho ya ndege na uzio wa ndani.

Miundombinu mingine iliyojengwa ni barabara ya kiusalama ndani ya kiwanja, maegesho ya magari.

“Kwa sasa kazi iliyobaki iliyobaki ni uwekaji wa taa ya kuongozea ndege ili kuwezesha kiwanja hicho kufanya kazi masaa 24 ambapo kwa sasa kinafanya masaa 12 Tu,” amesema.

Kazi nyingine iliyobaki ni ujenzi wa matenki ya kuhifadhia maji ambayo pia yatatumika kudhibithi majanga.

Kukamilika kwa kazi ya ukarabati na upanuzi katika kiwanja hicho utawezesha ndege kubwa zikiwemo za Airbus 320 na Boeing 787 Dreamliner kutua katika kiwanja hicho.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x