Umeme wawanyima usingizi nishati

SINGIDA: NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema watumishi wa wizara hiyo hawapati usingizi tangu walipopewa maagizo na Rais Samia Suluhu Hassan ya kumaliza changamoto ya upungufu wa umeme katika maeneo mbalimbali nchini.-

Kapinga ameyasema hayo leo Oktoba 17, 2023 kwenye ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan mkoani Singida.

“Ndani ya wiki hizi mbili kila asubuhi Waziri wa Nishati Dk Doto Biteko anafuatilia matengenezo ya mtambo wa Ubungo II wa Megawati 43, kila asubuhi anahakikisha na kusimamia, ili ndani ya wiki mbili megawati 43 ziwe zimerudi.

“Pia tunasimamia mradi wa Bwawa la Julius Nyerere kwa weledi mkubwa mno, kwa sasa tumeshafikia asilimia 92.74 tunataka kufikia mwezi Januari tuanze majaribio ya bwawa letu ili tumalizie changamoto ya umeme,” amesema Kapinga.

Amesema tayari wamepeleka umeme vijijini kwa asilimia 90 na wanaamini kufikia mwezi Juni 2024 watakuwa wamekamilisha vijiji vilivyosalia.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Mpango wa Kujitathmini Kiutawala Bora Barani Afrik
Mpango wa Kujitathmini Kiutawala Bora Barani Afrik
1 month ago

Mpango wa Kujitathmini Kiutawala Bora Barani Afrika (APRM)

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x