Ummy: Acheni matumizi holela ya dawa

TANGA: Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameitaka jamii kuacha matumizi holela ya dawa za antibiotik ili kuepuka usugu wa vimelea vya magonjwa.

Ummy ameyasema hayo katika mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa jamii kuhusu kuimarisha huduma za afya ngazi ya msingi kwa ushirikiano wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Odo Ummy Foundation pamoja na Taasisi ya Apotheker ili kuwajengea uelewa wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazo ikabili jamii hususani katika sekta ya afya.

“Sasa hivi kuna matumizi yasiyo sahihi ya dawa za antibiotik; mtoto ameumwa tumbo kidogo la kuharisha mzazi unaenda duka la dawa unanunua dawa za antibiotik matokeo yake tumesababisha usugu wa vimelea vya magonjwa hali inayo pelekea kila dawa za anti kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi,” amesema Ummy na kuongeza

” Mtoto akiharisha apewe ORS – Zink. Antiobiotik ni hadi aandikiwe na Daktari,”amesisitiza

Amesema, kwa sasa matumizi ya dawa za antibiotik yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 65.

“Shirika la Afya Duniani (WHO) lina sema kwa wagonjwa wanao lazwa tusifike asilimia 30 sasa tupo asilimia 65,” amesema.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Sera wa Apotheker, Dk Suleiman Kimatta amesema magonjwa mengi kama vile ukimwi,kifua kikuu,malaria kuna vimelea vinavyo sababisha magonjwa hayo hivyo ni muhimu kumeza dawa sahihi ili kuweza kuua vimelea kwani ukitumia dawa kiholela inapelekea kimelea kuwa sugu na kuhatarisha afya yako pamoja na kifo.

Habari Zifananazo

Back to top button