Ummy atoa maagizo kwa wamiliki wa maduka ya dawa
ARUSHA; Waziri Afya ummy Mwalimu ametoa onyo kali kwa wafamasia na wamiliki wa maduka ya dawa kutotoa dawa bila kuangalia cheti cha daktari kwa kuwa kufanya hvyo ni kuendeleza tatizo la usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa na kuhatarisha afya za watu.
Waziri Ummy amesema hayo leo Novemba 17,2023 wakati akifunga kongamano la tatu la usugu wa vimelea dhidi ya dawa na kufungua rasmi wiki ya uhamasishaji na uelimishaji jamii juu ya matumizi sahihi ya dawa inayoanza Novemba 18 hadi 24,2023
“Nataka wafamasia wote nchini kuacha mara moja tabia ya kutoa dawa ikiwemo za antibiotiki bila cheti cha daktari nikimkamata mtu siku moja nitampiga faini kubwa kama sio kumfungia duka kabisa”Amesema Waziri Ummy
Aidha,Amesema atatuma timu kufanya kaguzi za kushtukiza kwenye maduka ya dawa,ambapo amesisitiza mfamasia atakaebainika kutoa dawa za antibiotiki bila cheti cha daktari atafikishwa mahakamani na atalipa faini kubwa
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa serikali ,Prof. Tumaini Naga amewaasa wataalamu wa kilimo, Uvuvi, na mifugo na Afya kwa kuzingatia dhana ya mwaka huu ya kongamano hilo kwa kuendelea kuboresha njia za mapambano ya tatizo la usugu na vimelea dhidi ya dawa na kutoa elimu ya uelewa kwa jamii ili kufikia mpango huo.