Umuhimu wa uchumi stahimilivu kukabili majanga

DAR ES SALAAM: Kwa miaka mingi, utajiri umehusishwa na mali zinazoonekana na kushikika kama vile ardhi, mifugo, au majengo.
Vitu vyote hivi vimekua vikitafsirika kama alama ya uchumi wa mtu. Tunapotazama uchumi siku hizi, utajiri wa kweli hupimwa na ustahimilivu wa kifedha hasa katika majanga ikiwemo uwezo wa kukabiliana na changamoto za kimaisha bila kuwa na shaka lolote wala kutetereka kiuchumi.
Matukio ya hivi karibuni ikiwemo janga la UVIKO 19 umeonyesha umuhimu wa kuwa na uchumi ulio stahimilivu ikiwa ni pamoja na kuwekeza vyema.
Janga hili pia limeonyesha umuhimu wa kupata pesa kupitia uwekezaji wa kimkakati wa kiuchumi ambao ni muhimu katika kukabiliana na majanga yanayoweza kujitokeza muda wowote.
Mtazamo huu unaenda mbali zaidi na kusisitiza uwekezaji wenye kutoa ulinzi wa fedha zako hasa kupitia bima za maisha na pensheni ambazo kwa pamoja zimekua suluhisho kubwa la kulinda maisha ya mteja pamoja na kutoa ulinzi wa uhakika na ukuaji wa fedha zake.
Huduma mbalimbali za bima za maisha ikiwemo pensheni binafsi inampa mtu nafasi ya kuwekeza pesa zake kidogo kidogo na kumuhakikishia ongezeko la fedha hizo baada ya muda.
Elimu ya bure ya uwekezaji pia imeendelea kutolewa ili kumpa mtu sababu za kuwekeza kupitia bima za maisha na hii hukuza desturi ya uwekezaji katika jamii.
Kwa mfano, Jubilee Life Insurance inatoa suluhisho la uwekezaji na ukuaji wa kipato cha mteja huku ikihakikisha ulinzi wa maisha ya mteja pamoja na wapendwa wake, hii inampa mteja amani kwa kujua kwamba hakuna janga au changamoto itakayokwamisha ndoto zake za kiuchumi.
Hillary Godson ni Afisa Mkuu wa Fedha Jubilee Life Insurance



