Korosho Marathon 2025 yaiva

MTWARA; BODI ya Korosho kwa kushirikiana na Kampuni ya Makanjiro imeandaa Korosho Marathon 2025 kwa nia ya kuchangisha fedha kununua mashine za kubangua korosho kwa ajili ya wabanguaji wadogowadogo vijijini.

Mkurungezi Mkuu wa bodi hiyo Francis Alfred, amesema hayo wakati wa uzinduzi wa maandalizi ya Korosho Marathon ambayo yamepangwa kufanyika 29 Novemba mwaka huu.

Amesema hatua hiyo imelenga kuhamasisha ubanguaji wa korosho ndani ya nchi katika kufikia lengo la serikali la kubagua korosho zote nchini ifkapo 2030.

Francis amesema wabanguaji wadogowadogo wakiwemo wakulima wamekuwa wakinbagua korosho kwa kutumia mashine za kawaida (manila), ambazo zinachukua muda mwingi kubangua.

“Mwaka huu tumepanga kuwapa wakulima ambao wamejiunga kwenye vikundi kwa ajili ya kuanza kubangua korosho, na Marathon ni ya sehemu ambayo tunategemea kupata fedha, kwa ajili ya kununua hizo mashine,”amesema.

Amesema bodi kwa mwaka huu imetanga Sh milioni 200 kununua mashine.

Mbio hizo za marathon zitanguliwa na maonesho mbalimbali ya bidhaa za korosho na shughuli nyingine za korosho kuanzia Novemba 24.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button