Umuhimu wa utalii katika kukuza uchumi jumuishi

KWA kuwa utalii ni miongoni mwa sekta kubwa na zinazokua kwa kasi duniani kote; inatoa ajira, inakuza tamaduni na kuchangia kwa kiwango kikubwa katika pato la taifa, wadau wa sekta hii wamehimizwa kuwekeza katika utalii endelevu katika nyanja mbalimbali za sekta hiyo.

Hatua hiyo ni muhimu katika kuzalisha ajira, kukuza utamaduni na kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye pato la taifa.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni jijini Arusha wakati wa Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Profesa Eliamani Sedoyeka alipozungumza katika ufunguzi wa Mkutano na Maonesho ya Utalii wa Kimataifa wa Arusha (AITC) 2025 uliokuwa na kaulimbiu: ‘Utalii na Mabadiliko Endelevu.’

SOMA: Tanzania yang’ara utalii duniani

Kwa mujibu wa Profesa Sedoyeka, wadau wa utalii wanapaswa kuwekeza katika utalii rafiki kwa mazingira na tamaduni kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

“Mkutano huu si tu umekuja wakati mwafaka, bali pia wa ni kihistoria kwani umeleta pamoja sauti za wadau wa ndani na kimataifa kujadili moja ya masuala muhimu ya uwekezaji katika utalii endelevu,” anasema.

Anaongeza: “Kaulimbiu ya mkutano wa mwaka huu, inaakisi changamoto na fursa kwa wakati mmoja. “Inatukumbusha kwamba sekta ya utalii haina budi kubadilika kwa namna ya kuheshimu mazingira, kuwezesha jamii na kukuza uchumi jumuishi.”

Anasema uendelevu wa utalii hauwezi kuchukuliwa kirahisi kwa kuwa mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira na kupotea kwa urithi wa kitamaduni yanahitaji kushughulikiwa kwa dharura na watunga sera, wawekezaji, watafiti na jamii kwa ujumla.

Profesa Sedoyeka anasema katika mkutano huo kuwa, IAA imejipanga kuunga mkono utalii si kama taaluma pekee, bali kama mhimili wa maendeleo ya taifa.

“Tumewekeza katika mafunzo, utafiti na huduma za ushauri zinazoshughulikia changamoto halisi katika utalii, ukarimu na maendeleo endelevu,” anasema.

Anaongeza: “Kupitia ushirikiano wetu na mashirika ya serikali, wadau wa sekta binafsi pamoja na washirika wa kimataifa, tunahakikisha wahitimu wetu si tu wanaajirika, bali pia wako tayari kuongoza ubunifu katika utalii endelevu.”

Anasisitiza umuhimu wa ushirikishwaji katika utalii, akibainisha kuwa jamii zinazozunguka hifadhi za taifa na maeneo ya urithi wa kitamaduni zinapaswa kuwezeshwa na kufaidika moja kwa moja kutokana na mapato ya utalii.

Hatua hiyo anasema inaleta umiliki, fahari na ari ya kuhifadhi rasilimali hizo. Kuhusu teknolojia, Profesa Sedoyeka anasema ipo haja ya kuikumbatia kama chachu ya suluhu endelevu.

Anasema utalii endelevu unahitaji sera thabiti na kanuni madhubuti zinazohamasisha uwekezaji wenye uwajibikaji, kukuza miundombinu rafiki kwa mazingira na kulinda urithi wa asili na wa kitamaduni.

“Arusha imekuwa kitovu cha majadiliano ya kimataifa. Kuandaa Mkutano na Maonesho ya Utalii wa Kimataifa wa Arusha (AITC) 2025, kunathibitisha nafasi ya jiji hili si tu kama mji mkuu wa utalii wa Tanzania, bali pia kituo cha kubadilishana maarifa na ubunifu,”anasem Profesa Sedoyeka.

Anasema utalii ni miongoni mwa sekta kubwa na zinazokua kwa kasi duniani kote na kwamba, pia inatoa ajira, inakuza ubadilishanaji wa tamaduni na inachangia kwa kiwango kikubwa katika pato la taifa.

Anasema nchini Tanzania, sekta hii inachangia takribani asilimia 20 ya Pato la Taifa na kuajiri maelfu ya watu.

Kwa upande wake Mhadhiri Mwandamizi, Mtafiti na Mshauri katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, Dk CRN Raphael anasema wadau wa utalii nchini wanapaswa kubadilika kutoka kutumia mbinu za kiasili za uendeshaji wa utalii na ukarimu.

Anasema badala yake, waende katika mbinu za kisasa kwa kukumbatia teknolojia za kidijiti.

“Ulimwengu unabadilika kutokana na teknolojia na utandawazi. Moja ya mabadiliko makubwa tunayoshuhudia sasa ni mabadiliko ya kidijiti,” anasema.

Dk Raphael anaongeza: “Teknolojia za kidijiti zinagusa utalii na ukarimu sambamba na sekta nyingine. Moja ya njia za kubadilisha utalii na kunufaika na fursa zilizopo ni kupitia matumizi ya teknolojia hizi.”

Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Utalii ya DeMi Tours Africa, Caudence Ayoti anasema mkutano huo umempa nafasi ya kujenga mtandao na wadau wengine wa utalii.

Anabainisha kuwa, kampuni yake imejikita katika kuwasaidia wanawake ikiwa ni pamoja na kuwapatia mafunzo kuhusu masuala ya utalii ili wajikwamue kiuchumi.

Kuhusu uzoefu wake katika utalii nchini Canada, Australia na Marekani, Scott Slessor kutoka Sasglass, Nova Scotia nchini Canada anasema nchini Canada, asilimia 66 ya biashara zinazounga mkono utalii ni biashara ndogo na za kati.

Anasema nchini, Australia ni asilimia 70 na nchini Marekani hali inalingana na Canada.

“Kwa Tanzania sijui hali ikoje, lakini nina uhakika inaweza kuwa asilimia 50 au 60 au 70 ya biashara zinazounga
mkono utalii ni biashara ndogo,” anasema Slessor.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  3. I honestly didn’t expect much when I first tried this, but here I am making around 6,854/USD a month just by working online a few hours a day from home. It’s not a get-rich scheme, just something steady that’s been working for me quietly in the background. If you’ve been looking for something consistent like I was, here’s what I started with:
    👉 https://www.jobs67.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button