UN yaipinga Israel kuongeza mapigano Gaza

NEW YORK: UMOJA wa Mataifa umesema unapinga vikali mpango wa Israel wa kuongeza operesheni zake katika Ukanda wa Gaza.

Akizungumza mjini New York kuhusu suala hilo, Msemaji wa Umoja huo, Farhan Haq, alisema wanapinga kwa nguvu zote ongezeko la machafuko katika eneo hilo. “Hatuwezi kushuhudia mzozo huu ukiendelea kuondoa maisha ya watu,” alisema Haq.

Taarifa za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa, hadi sasa, mzozo katika Ukanda wa Gaza umesababisha vifo vya zaidi ya watu 60,000 katika kipindi cha miaka miwili ya mapigano. SOMA: Merz: Tunakwenda Gaza kutafuta majibu

Haq aliongeza kuwa, katika mazingira ya sasa, ukiukwaji wa haki za binadamu unaendelea kutesa maelfu ya watu, na kuna hatari ya vifo zaidi endapo mzozo huo utaendelea.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button