United, Spurs Super Sunday

MAN United itaendelea kukosa huduma ya wachezaji, Victor Lindelof, Luke Shaw, Tyrell Malacia na Leny Yoro kuelekea mchezo wa EPL leo dhidi ya Tottenham Hotspurs, huku kiungo Mason Mount aliyerejea mchezo wa Europa dhidi ya Twente FC ataendelea kuwa sehemu ya kikosi.

Shirika la Habari BBC, lilimnukuu meneja wa Man United, Erik ten Hag kuwa baada ya kurejea Mason Mount hakuna majeruhi mpya.

Wakati United ikiingia katika mchezo huo na baadhi ya wachezaji wak muhimu, Tottenham bado wana wasiwasi wa utimamu wa mshambuliaji wao tegemeo, Son Heung-min, aliyelazimika kutolewa nje dhidi ya Qarabag kwenye mchezo wa Europa.

Kocha wa Spurs, Ange Postecoglou alithibitisha “kila mtu yuko sawa” baada ya ushindi wa Alhamisi wa Ligi ya Europa, huku Wilson Odobert na Richarlison wakisalia nje kwa muda mrefu.

Mchezo wa mwisho uliopigwa Old Trafford msimu uliopita, timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.