Uongozi RT una mengi ya kufanya

MCHEZO wa riadha ni moja ya michezo inayofanya vizuri sana kuliko mchezo wowote katika nyanja ya kimataifa hapa nchini.
Wengi hawajui na ukiwaambia hivyo, watakwambia ni mchezo wa soka. Ni kweli mchezo wa soka ni maarufu zaidi hapa nchini lakini haufanyi vizuri kama unavyofanya ule wa riadha.
Takwimu zinaonesha kuwa Tanzania imefanya vizuri zaidi katika mchezo huo kimataifa kuliko mchezo wowote ule, iwe kwa mchezaji mmoja mmoja au timu tangu miongo mingi imepita.
Mfano, mwaka 1974 mwanariadha nguli, Filbert Bayi alishinda medali ya dhahabu katika Michezo ya Jumuiya ya Madola yalipofanyikia Chrischurch, New Zealand.
SOMA: Kishindo cha Wanariadha waliofanya vizuri Japan
Bayi sio tu alitwaa medali ya dhahabu, pia alifanikiwa kuivunja rekodi ya dunia ya mbio za meta 1,500 aliyodumu nayo kwa takribani miaka mitano, hadi ilipovunjwa na Muingereza Sebastian Coe.
Katika michezo hiyo, Cleva Kamanya alipata medali ya shaba katika mbio za meta 400.
Tanzania iliendelea kutamba katika Michezo ya Olimpiki mwaka 1980 Moscow, Urusi. Ilipata medali mbili za fedha kutoka kwa Seleman Nyambui na Bayi katika mbio za meta 5,000 na 3,000 za kuruka gogo na maji.
Zakayo Malekwa alipata medali ya shaba katika Michezo ya Jumuiya ya Madola iliyofanyika Brisbane, Australia
mwaka 1982 pamoja Juma Ikangaa aliyekuwa wa tatu katika mchezo wa marathoni.
Pia, Tanzania iliwahi kupata medali katika mbio za meta 5,000 na 10,000 kwa nyakati tofauti na kuifanya kutamba na kuogopwa kwa ukali.
Sio Michezo ya Jumuiya ya Madola pekee na Olimpiki pia wanariadha wake wa mbio ndefu walitamba katika mbio mbalimbali kubwa walizoalikwa, wamewahi kufanya maajabu na kuleta heshima kubwa.
Miaka ya hivi karibuni, Tanzania imeendelea kutamba lakini katika mbio za marathoni na kusahau michezo mingine ambayo nayo tulikuwa tunatamba nayo.
Uongozi mpya wa Riadha Tanzania (RT), chini ya uongozi wa Roghat Akhwari una kazi kubwa ya kufanya.
Kwanza, kuhakisha watu au wanariadha wanaondoa dhana kuwa mchezo wa riadha wenye pesa za haraka haraka ni ule wa marathoni tu, kumbe na mingine ipo. Hivyo, watilie mkazo kwenye michezo mingine.
Pili, RT ihakikishe inaanza kuwaendeleza watoto na vijana katika mchezo huo, wakianza na mbio fupi, miruko na mitupo ili kuwa mahiri hata katika michezo hiyo pia.
Michezo hiyo imekuwa na zawadi ya fedha nyingi na World Athletics (WA) imeanzisha mashindano ya mara kwa mara kama ile ya Grand Prix.
Zawadi za washindi wa Mashindano ya Riadha ya Dunia zilikuwa sawa kwa michezo yote, kuanzia marathoni hadi mbio fupi, miruko na mitupo.
Pia, uongozi mpya wa RT uutangaze zaidi mchezo huo siku hadi siku ili ujulikane zaidi na wengi waupende kuliko
sasa ambapo wengi wanajua riadha ni kukimbia marathoni tu, hakuna mchezo mwingine.
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com