‘Urani ya Namtumbo, mwanga mpya Tanzania kuelekea uchumi wa kisasa’
CHINI ya ardhi ya Mkuju wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma kumelalia utajiri mkubwa usioonekana kwa macho ya kawaida madini ya urani.
Ni madini adimu yenye nguvu kubwa, yanayotumika kutengeneza nishati ya nyuklia, nishati safi inayotazamwa duniani kote kama suluhisho la upungufu wa umeme na kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Katika eneo la Mkuju, shughuli za maandalizi ya mradi mkubwa wa uchimbaji wa urani zimechukua kasi mpya. Mradi huo unaoendeshwa na kampuni ya Mantra Tanzania Limited, unatajwa kuwa miongoni mwa miradi mikubwa zaidi ya urani duniani ambayo bado haijaendelezwa kikamilifu.
Madini ya urani ya Namtumbo ni urithi wetu Watanzania ambao umeleta matumaini mapya, uchumi, ajira, na mabadiliko ya kijamii yanayoweza kuandika ukurasa mpya katika historia ya Tanzania. Nguvu ya kijani chini ya ardhi ya Ruvuma Tanzania ni miongoni mwa nchi chache barani Afrika zenye hifadhi kubwa ya madini ya urani.
Watafiti wa jiolojia waligundua madini hayo mwaka 1996, na tangu hapo, eneo la Mkuju limekuwa kitovu cha utafiti na maandalizi ya uchimbaji.

Ruvuma.
Kwa mujibu wa taarifa za Mantra Tanzania, mradi wa Mkuju unaweza kutoa urani kwa zaidi ya miaka 15 mfululizo, na kwa kiwango hicho, Tanzania inaweza kuchangia asilimia 4 ya madini yote ya urani duniani na takribani asilimia 20 ya uzalishaji wa Afrika.
Lakini nini hasa kinachofanya Tanzania kuwa kivutio kwa wawekezaji katika sekta hii nyeti? Kwanza, ni sera rafiki za Serikali katika sekta ya madini ambazo zimeboresha mchakato wa upatikanaji wa leseni na kodi, jambo lililovutia kampuni za kimataifa kama Mantra kuwekeza nchini. Pili, Tanzania ina miundombinu thabiti, ikiwemo Bandari ya Dar es Salaam na barabara kuu zinazorahisisha usafirishaji wa malighafi.
Zaidi ya hayo, nguvukazi ya Watanzania hasa vijana waliohitimu vyuo vya jiolojia, uhandisi na teknolojia, imekuwa rasilimali muhimu katika uendelezaji wa miradi hii mikubwa. Jamii za Namtumbo zaanza kuvuna Kampuni ya Mantra Tanzania haijabaki nyuma katika kushirikisha jamii za wazawa.
Kupitia programu za kijamii, kampuni imewekeza katika mafunzo ya usalama, ajira, na miradi ya kijamii katika vijiji vya Mtonya, Likuyu Seka na Likuyu Mandela. Meneja Uendelevu wa Mantra Tanzania, Majani Wambura anasema zaidi ya vijana 200 wamepata mafunzo ya kiufundi na ajira za muda, huku wanawake wakihusishwa katika shughuli za huduma, upishi na usafi katika maeneo ya mradi.
“Kila kitu tunachofanya kinazingatia usalama, mazingira, na maendeleo ya jamii, tunataka mradi huu uwe mfano wa uwajibikaji wa kijamii barani Afrika,” anasema Wambura. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Ahmed Abbas, anasema mradi huu ni nguzo mpya ya uchumi wa mkoa na utafungua fursa nyingi kwa wananchi.
Urani na Mazingira
Urani ni madini yenye nguvu lakini yanayohitaji umakini mkubwa katika uchimbaji wake. Mantra Tanzania imesisitiza kuwaUrani ni madini yenye nguvu lakini yanayohitaji umakini mkubwa katika uchimbaji wake. Mantra Tanzania imesisitiza kuwa shughuli zote zinafanywa kwa viwango vya kimataifa vya usalama.
Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kupunguza matumizi ya maji na kemikali katika uchakataji, kuchakata na kurejesha maji yanayotumika viwandani na ufuatiliaji wa mazingira unaohusisha jamii moja kwa moja.

“Tunataka kuhakikisha hakuna athari hasi kwa afya ya binadamu wala mazingira,” anasema Majani na kuongeza: “Tunatumia teknolojia ya InSitu Recovery (ISR), mbinu ya kisasa inayopunguza uharibifu wa ardhi.”
Ahadi ya serikali
Wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha majaribio cha kuchenjua urani katika kijiji cha Likuyu Agosti 2025, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alieleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa dira ya Tanzania ya kujitegemea kiuchumi kupitia viwanda.
“Tanzania itakuwa kwenye ramani ya dunia kama miongoni mwa wazalishaji 10 wakubwa wa urani, na mradi huu utaongeza ajira, mapato ya kigeni na maendeleo ya sekta nyingine,” alisema Rais Samia. Tathmini inaonesha kuwa mradi wa Mkuju una thamani ya uwekezaji wa Dola za Marekani bilioni 1.2 (takribani Sh trilioni 3), utakaotoa ajira 3,500 hadi 4,000, zikiwemo ajira za kudumu 750.
Kwa upande wake, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, anasema kuwa Tanzania sasa ni miongoni mwa nchi tano barani Afrika zenye miradi mikubwa ya uchenjuaji wa urani, hatua inayoongeza hadhi ya nchi katika ramani ya dunia ya nishati safi.
Faida zinazogusa kila Mtanzania
Mbali na ajira na uwekezaji wa fedha za kigeni, mradi wa urani wa Namtumbo unatarajiwa kuchochea maendeleo katika sekta nyingine nyingi. Mapato ya madini hayo yatawezesha ujenzi wa miundombinu kama barabara, shule na hospitali, kukuza sekta ya elimu kwa ufadhili wa wanafunzi wa masomo ya sayansi na kuongeza mapato ya serikali kwa kodi na tozo za uchimbaji.
Kwa mujibu wa wachambuzi wa uchumi, mradi huu unaweza kuongeza asilimia 1.5 hadi 2 ya pato la Taifa (GDP)
kila mwaka mara utakapokuwa kwenye uzalishaji kamili.
Maono ya Muda Mrefu
Maono ya Mantra na Serikali ni kuendeleza madini haya kwa uwajibikaji wa kijamii, kiuchumi na kimazingira. Wataalamu wanasisitiza kuwa urani ni ‘dhahabu ya kisasa’ inayoweza kuleta mageuzi makubwa ikiwa itasimamiwa ipasavyo.
Kampuni ya Mantra inasisitiza kuwa jamii lazima zinufaike moja kwa moja kupitia huduma za kijamii, mikopo midogo, ajira na uwezeshaji wa miradi ya wanawake na vijana. “Tunajenga urithi, tunataka vizazi vijavyo vikumbuke urani ya Namtumbo kama chimbuko la maendeleo, si kama doa kwenye historia,” anasisitiza Majani.
Mwanga mpya kutokaNamtumbo
Kutoka kwenye ardhi tulivu ya Ruvuma hadi kwenye ramani ya dunia, urani ya Namtumbo inasimama kama ishara ya mwelekeo mpya wa uchumi wa Tanzania, uchumi unaotegemea teknolojia, nishati safi na uwekezaji endelevu.
Ikiwa mradi huu utatekelezwa kwa uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji wa wananchi, basi urani ya Namtumbo haitabaki tu kuwa makala ya kuvutia magazetini, itakuwa hadithi ya kweli ya Tanzania mpya inayoinuka kwa nguvu za rasilimali zake.
Urani ya Namtumbo ni mwanga wa matumaini, injini ya viwanda na nguzo ya mustakabali wa taifa lenye ndoto za kujitegemea.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com
Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
.
More Details For Us →→ http://www.big.income9.com