URUSI: Kikosi cha kijeshi DPRK kinapungua

URUSI : WANAJESHI wa Korea Kaskazini wanazidi kupungua kwa asilimia 40 baada ya miezi mitatu ya mapigano katika mkoa wa Kursk, Urusi.
Kati ya wanajeshi 11,000 waliotumwa, 4,000 wameripotiwa kujeruhiwa, kuuawa au kukamatwa, huku 1,000 wakiendelea kudhaniwa kuwa wameuawa kufikia mwezi Januari.
Takwimu hizi zinatoa picha mbaya kwa Korea Kaskazini, ikiwa hasara hizo zitathibitishwa.
Hali hii inakuja wakati waasi wa Korea Kaskazini, wanaoungwa mkono na Urusi, wakishirikiana na Rais Vladimir Putin kujaribu kutimua majeshi ya Ukraine kutoka maeneo ya Urusi, huku Ukraine ikifanya mashambulizi ya kushtukiza mkoani Kursk mwezi Agosti. SOMA: Jeshi la Korea Kaskazini laingia Urusi
Wanajeshi wa Korea Kaskazini wanaripotiwa kuwa na mafunzo duni na wanapigana kwa mbinu za zamani, jambo linalowafanya kuwa katika hatari kubwa ya kushambuliwa na ndege zisizo na rubani za Ukraine.
Kanali Hamish de Bretton-Gordon, kamanda wa zamani wa jeshi la tanki la Uingereza, alisema: “Hawa ni wanajeshi wasio na mafunzo ya kutosha wanaoongozwa na maafisa wa Urusi ambao hawawajui.”



