Bandari ya Mtwara yazidi kung’ara kimataifa

MTWARA : SERIKALI ya Urusi imeonyesha nia ya kutumia Bandari ya Mtwara kusafirisha bidhaa zake na kuzisambaza katika nchi jirani na Tanzania, ikiwemo kusafirisha korosho kwenda soko la Urusi.

Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Andrey Avetisyan, amesema hayo wakati alipotembelea Bandari ya Mtwara kuangalia fursa za biashara na uwekezaji mkoani humo akiwa ameambatana na ujumbe kutoka ubalozi huo. Amesema Urusi ina bidhaa nyingi zinazoweza kusafirishwa kupitia bandari hiyo kwenda nchi za Afrika Mashariki na Kusini, ikiwemo mbolea na bidhaa za nishati.

Kwa mujibu wa Avetisyan, Bandari ya Mtwara imeboreshwa na ina nafasi kubwa kutokana na eneo lake la kijiografia, kwani inapakana na nchi ambazo hazina bahari, hivyo ni rahisi kuhudumia shehena kutoka Urusi. Kwa upande wake,Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala, amepongeza hatua hiyo akisema itasaidia kutangaza bandari kimataifa na kuinua uchumi wa mkoa.

Balozi Avetisyan pia alitembelea Kongani la Viwanda la Mranje na kufanya mazungumzo na viongozi wa mkoa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Alfred Francis. SOMA: Tanzania, Urusi kushirikiana utalii

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Google pays $300 on a regular basis. My latest salary check was $8600 for working 10 hours a week on the internet. My younger sibling has been averaging $19k for the last few months, and he constantly works approximately 24 hours. I’m not sure how simple it was once I checked it out.

    This is my main concern………………. http://Www.Cash43.Com

  2. I just got paid $22k working off my laptop this month!** And if you think that’s cool, my divorced friend has twin toddlers and made over $22620 her first month. details on this website**Want the secret?** Copy this Website and choose HOME TECH OR MEDIA……..

    Here is I started_______ https://Www.CashHive1.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button