Usafiri treni ya mikoani wasitishwa

SHIRIKA la Reli (TRC) limesitisha huduma za usafiri wa treni, kutoka Dar es Salaam kuelekea katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Katibu, Kigoma, Shinyanga na Mwanza pamoja na mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Taarifa iliyotolewa leo Januari 18, 2024 na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa TRC, Jamila Mbarouk imeeleza sababu za kusitisha huduma hiyo ni kutokana na uharibifu wa miundombinu ya reli uliotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

“Wahandisi wanaendelea na matengenezo katika maeneo yaliyoathirwa na mvua.” Imeeleza taarifa hiyo.

Aidha taarifa imefafanua kuwa huduma hiyo inatarajiwa kurejea Januari 23 2024 baada ya kukamilika kwa matengenezo hayo.

Habari Zifananazo

Back to top button