Usafiri wa treni wasimama London

LONDON, UINGEREZA: MAMILIONI ya Wakazi wa London wanakabiliwa na changamoto kubwa ya usafiri kufuatia kuanza kwa mgomo wa siku tano wa wafanyakazi wa treni za chini ya ardhi, ulioshuhudia vituo kadhaa vikifungwa na huduma muhimu kukwama.

Mgomo huo ulianza jana Jumapili (Septemba 7, 2025) na tayari umesababisha usumbufu mkubwa, huku Shirika la Usafiri la London (TfL) likionya kuwa huduma zitakuwa chache mno au kutokuwepo kabisa wiki hii endapo mzozo huo hautapatiwa suluhu. SOMA: Watu 13 wapoteza maisha ajali ya treni India

Chama cha Wafanyakazi cha RMT kimeitisha mgomo huo kikishinikiza nyongeza ya mishahara na mazingira bora ya kazi, baada ya kukataa pendekezo la ongezeko la asilimia 3.4 lililotolewa na TfL. Madereva wa treni pamoja na wahandisi wa matengenezo pia wamejiunga katika mgomo huo, hali inayoongeza shinikizo kwa serikali na waajiri.

Habari Zifananazo

9 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button