USAILI wa watiania wa kugombea wa nafasi za juu za uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umefanyika ikiwa ni maandalizi kuelekea uchaguzi nafasi hizo unaotarajiwa kufanyika kesho.
Usaili huo umefanyika jana katika Makao Makuu ya chama hicho, Mikocheni, Dar es Salaam ambapo watia nia waliofanyiwa usaili huo ni wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti Bara na Zanzibar na Wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho.
Watia nia nafasi ya uenyekiti ni Freeman Mbowe anayetetea nafasi yake, Tundu Lissu na Charles Odero. Aidha, watia nia wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara ni John Heche na Ezekia Wenje na wagombea Makamu Mwenyekiti Zanzibar ni Hafidh Ali Saleh, Said Issa Mohamed, Said Mzee Said na Suleiman Makame Issa. Chadema ilianza uchaguzi wa ndani Januari 13 mwaka huu kwa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA), Baraza la Wazee Chadema (BAZECHA) na Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA)